Na Khadija Kalili
KAMPENI ya kuhamasisha watanzania kupata chanjo ya UVIKO19 inayokwenda kwa jina la 'Niko' imezinduliwa leo Julai 31, 2022 jijini Dar es Salaam ambapo itakuwa ikiendeshwa na Taasisi isiyo ya kiserikaki ya Access Challenge yenye maskani yake nchini Marekani.
Taasisi hiyo ambayo tayari wako barani Afrika kwa miaka 15 sasa, pia waliwahi kufanya kampeni za kutokomeza magonjwa ya Ebola, Malaria No More, Pneumonia na mengineyo.
Jamii imeaswa kujitokeza kuchanja kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba.
'One by One COVID 19 Vaccinetion Target 2030 (Niko Tayari) imezinduliwa huku lengo likiwa ni kuutokomeza ugonjwa huu ifikapo mwaka 2030.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mratibu wa Elimu ya Afya kwa umma kutoka Wizara ya Afya Peter Mabwa amesema lengo kubwa la Serikali katika kampeni hii ni kuhakikisha kuwa nchi inakuwa salama dhidi ya magonjwa na dharura mbalimbali za kiafya huku akiahidi kuwafikia wananchi na kuwapatia taarifa kwa wakati na kuwapa elimu sahihi ili kuepuka upotoshaji unaojitokeza kuhusu UVIKO19 na dharura nyinginezo za kiafya.
Mabwa amesema kuwa kwa niaba ya Wizara ya Afya wanawashukuru Jakaya Kikwete Foundation, Access Challenge, Africa CDC, Clouds Media Group na Shirika la FH360 pia wanatambua mchango wao katika mapambano dhidi ya COVID 19.
Mabalozi wa kampeni hii ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Nickson Simon almaarufu kwa jina la Nikki wa Pili amesema kuwa Wilaya yake imefanikiwa kwa kiwango cha juu katika mwamko WA kuchanja kwa sababu zoezi hili lilisimamiwa kwa umoja na ushirikishwaji kutoka kila Idara na maeneo yote Wilayani Kisarawe.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Zuwena Mohammed almaarufu kwa jina la 'Shilole' aliwahamasisha wananchi kujitokeza kuchanja chanjo ya UVIKO 19 kwa sababu ugonjwa huu bado upo nchini na duniani kote.
"Niwatoe hofu siyo kweli kwamba chanjo hii ina madhara kuna wagonjwa kama,sukari, wajawazito na wote wenye magonjwa mengine wanaweza kuchanja hii ni kwa mujibu wa Wizara ya Afya"alisema Shilole.
"Lengo la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ni kutuletea kinga wananchi wake mimi nimechanja na ninatembea na cheti changu na huwa nakionyesha pindi ninapokuwa jukwaani ninapokuwa nahamasisha kuhusu umuhimu wa kuchanja nawaonyesha wananchi ili waweze kuamini kwamba kile ninacho kisema "amesema Shilole.
"Awali ya yote tunatakiwa tumshkuru Rais wetu Mama Samia Suluhu aliyetuletea chanjo hizi bure hivyo tusimuangushe tukachanje hakuna mama ambaye anaweza kuleta sumu nyumbani iangamize watoto wake hivyo Rais wetu hawezi kuleta njanjo itakayo angamiza Taifa lake"alisema Shilole.
Kwa upande wake Massoud Kipanya ambaye pia ni balozi wa COVID 19 ameongeza kwa kusema kuwa anawashangaa baadhi ya watu ambao wanaleta maneno ya kupotosha kwamba chanjo zina madhara huku akisema kuwa yeye amechanja huu ni mwaka wa pili lakini hajapatwa na madhara yeyote na ushahidi huo upo hata kwa watu wengine ambao wamepata chanjo hiyo.
"Watu waache kudanganya jamii kuwa chanjo inapunguza nguvu za kiume mimi nimechanja na niko imara" alisema Kipanya.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Nickson Simon maarufu kwa jina la Nikki wa Pili akizungumza kwenye uzinduzi huo jijini Dar Es Salaam leo Julai 31, 2022.
Kutoka Kushoto ni Balozi wa kampeni NIKO TAYARI, Zuwena Mohammed Maarufu kama Shilole akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya hiyo jijini Dar es Salaam leo Julai 31,2022. kulia ni Masoud Kipanya.
Picha ya Pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...