Kiboko dume ambaye kwa muda mrefu amekuwa akisumbua Wananchi wa Kata ya Mabilioni Wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro na kukwamisha shughuli za maendeleo kama kilimo, ufugaji na uchotaji wa maji katika Mto Pangani ameuawa kwa kupigwa risasi katika msako ulioongozwa na vikosi kutoka TAWA na Kiboko huyo aliyepewa jina la Babu ambaye ameua jumla ya Watu 6, zaidi ya ng’ombe 8, punda na mbuzi tangu mwaka 2017 alikuwa akihusishwa na imani za kishirikina kwani jitihada mbalimbali za kumdhibiti hazikufanikiwa katika kipindi chote

Tarehe 17 Juni 2022 kiboko huyo alimuua kwa kumshambulia Mwanaume mmoja aliyekuwa anakwenda shambani kumwagilia ndipo Mkuu wa Wilaya ya Same, Edward Mpogolo alipoagiza kuhakikisha kila mbinu zinatumika kumuua Kiboko huyo ili Wananchi warudi kufanya shughuli za maendeleo kwa amani

Baada ya kuanza msako kiboko huyo aliuawa tarehe 28 Julai 2022 saa 11 alfajiri baada ya kuweka mtego na kupigwa risasi ya kichwa na Mzee Ally Miraji Sengela (Hunter) aliyesaidiwa naz Mzee Fue Omary Ngerwa (Mvuvi na Mweka Mtego) kwa kushirikiana na wahifadhi wa TAWA.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...