*Huduma za jamii zimeimarika

 Na Mwandishi wetu, Mbeya

Chama Cha Mapinduzi kimesema licha ya Rais samia suluhu  Hassan huzungumza  polepole lakini vitendo vyake katika utekelezaji wa sera za maendeleo zimekuwa motomoto.

Pia, serikali yake kwa muda mfupi imeaminika na kuheshimika kikanda na kimataifa.

Matamshi hayo yametamkwa jana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana alipokuwa  katika Manispaa ya jiji la Mbeya.

Kinana alisema Rais Samia amekuwa kiongozi wa mfano ambaye kwa kipindi kifupi cha mwaka mmoja amekubalika katika medani za kidiplomasia huku akiaminiwa na taasisi za kimataifa.

Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025, alisema serikali yake imekuwa ikitekeleza  wajibu hatua kwa hatua na kuimarika kwa huduma za jamii.

"Rais Samia kiongozi mchapakazi asiye na majivuno. Kila uendapo utakutana na maendeleo ambayo hayakutegemewa yatokee  haraka. Anazungumza polepole lakini vitendo  ni vizito" Alisema Kinana.

Aidha, Makamu huyo Mwenyekiti alisema uongozi bora hupimaa kwa kutoa matokeo chanya ambayo kwa bahati nzuei kila sekta imepatiwa fedha  za kufanikisha miradi ya maendeleo.

"Kila eneo limegushwa katika maendeleo. Sekta za Maji,Afya ,elimu zimspatiwa fedha kusukuma mbele kwa muktadha wa kupunguza kero na  kumaliza changamoto sugu "Alisema Kinana

Hata hivyo kiongozi huyo aliwataka wanawake wengi zaidi kujitokeza katika kuwania nafasi za uongozi ili kukamilisha ndoto zao na kusema wanawake ni waaminifu na wasimamizi makini.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...