Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na mdau wa Dodoma Ndondo Cup 2022 Mh.Anthony Mavunde akiwa na Timu nzima ya Ndondo Cup wakiongozwa na Ndg. Yahaya Mohamed “Mkazuzu” leo wamekagua viwanja mbalimbali vitakavyotumika katika mashindano ya Ndondo Cup Jijijini Dodoma.
Mashindano hayo ya Ndondo Cup hatua ya mchujo yatahusishaTimu 32 na yanatarajiwa kuzinduliwa kesho katika uwanja wa Shell-Chamwino.
Akizungumza katika ukaguzi huo,Mbunge Mavunde amesema maandalizi ya ukarabati wa miundombinu ya viwanja hivyo umekamilika kwa asilimia kubwa ambapo katika hatua ya awali viwanja vikavyotumika ni Shell,Shule ya Msingi Chamwino na Shule ya Msingi Chang’ombe.
“Tumejipanga vizuri kutengeneza jukwaa la fursa kwa wachezaji wa Dodoma kupata fursa ya kutambulika ndani ya nchi na kimataifa kupitia vipaji vyao.
Kwasasa nguvu kubwa tutaiwekeza katika miundombinu ya viwanja ili kuvifanya vichezeke,pamoja na uwekaji wa magoli ya chuma katika viwanja zaidi ya 50 Jijini Dodoma.
Nitoe rai kwa wadau wa michezo wa Dodoma kuitumia fursa hii ya mashindano haya Dodoma Ndondo Cup kukuza michezo na kuendeleza vipaji vya vijana wa Dodoma”Alisema Mavunde
Naye Muandaaji wa Ndondo Cup Ndg. Yahaya Mohamed “Mkazuzu” amesema maandalizi ya uzinduzi wa 32 bora umekamilika na kuzitaka Timu zijiandae kwa ushindani mkubwa lakini wenye kuzingatia haki na usawa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...