Mbunge wa Jimbo la Songwe, Philip Mulugo.


Na Thobias Mwanakatwe


MBUNGE wa Jimbo la Songwe, Philip Mulugo, ameahidi kutoa Sh.milioni tatu kwa ajili ya kununulia injini ya boti ili kuwasaidia wavuvi wa Kijiji cha Iyovyo wanaovua samaki Ziwa Rukwa.

Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho katika mwendelezo wa ziara yake ya kuhamasisha maendeleo jimboni mwake, alisema atatoa fedha hizo mwezi Oktoba mwaka huu na kuwataka wavuvi nao waanze kuchonga mtubwi.

Mulugo aliwataka wavuvi ili waweze kupata mikopo zaidi inayotolewa na halmashauri pamoja na Benki ya NMB wajiunge katika vikundi ili waweze kutambulika na hivyo kuwa rahisi kukopesheka.

"Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameruhusu mapato ya ndani ya halmashauri ya asilimia 10 yatumike kukopesha vikundi vya akiba mama na vijana, na pia benki ya NMB inakopesha vikundi na dhamana inakuwa ni kazi mnayoifanya," alisema Mulugo..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...