Mhasibu Mkuu Fungu 50 wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Nuru Abdallahmed (wa kwanza kushoto) akisikiliza maelezo kuhusu mipango ya kitaifa kutoka kwa Mchumi kutoka Wizara hiyo Bw. John Uledi alipotembelea Banda la Wizara katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, jijini Dar es Salaam.



Kamishna Msaidizi wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Irene Rugemalila, akitoa elimu kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Sekta binafsi kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, jijini Dar es Salaam.



Msimamizi wa Fedha wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi(PPP), kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mwaidi Araba akitoa elimu kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Sekta binafsi kwa Bw. Avitus Mbona alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam jijini Dar es Salaam



Afisa Tehama kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Zuberi Msisi, akitoa elimu kuhusu Mfumo wa Kieletroniki wa Ulipiaji wa Huduma za Serikali (GePG) kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam jijini Dar es Salaam.

(Picha na WFM – DAR)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...