Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Songwe
MBUNGE wa jimbo la Songwe mkoani Songwe Mwalimu Philip Mulugo amemuomba Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahman Kinana kufikisha salamu yao kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwamba changamoto waliyonayo kwenye wilaya yao ni kukosa barabara za lami, hivyo wanaomba kujengewa barabara ya lami.
Akizungumza mbele ya Kinana wakati wa kikao cha ndani kilichowahusisha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Songwe Mulugo amesema kuwa tatizo lake ni moja tu.
“Salamu zangu kwanza tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa mambo anayomfanyia jimboni kwetu.Tumepiga hatua katika nyanja mbalimbali.
“Tatizo letu ni hili katika Mkoa wote wa Songe wilaya zote kuna barabara za lami lakini naombeni lami Wilaya ya Songwe, ni tatizo kubwa mno, nikipata lami Songwe hakuna shida, hakuna tatizo la kisiasa, kila kitu kipo shida yetu ni lami,”alisema Mulugo.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe Neema Mwandabila alitumia nafasi hiyo kumueleza Kinana kuwa wanawake wa Mkoa huo wanampa salamu nyingi Rais Samia kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kuwatumikia wananchi.“Tunaomba tufikishie salamu zetu kwa Rais Samia tunampenda na tunamuahidi kwamba tutamlinda nyakati zote.”
MBUNGE wa jimbo la Songwe mkoani
Songwe Mwalimu Philip Mulugo akiwa amepiga magoti mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania
Bara,Ndugu Abdulrahman Kinana akiomba amfikishie salamu yao kwa Rais Samia Suluhu
Hassan kuhusu changamoto ya barabara ya Lami waliyonayo kwenye wilaya yao,wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Julai 27,2022.PICHA NA MICHUZI JR-SONGWE.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...