Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Bondia wa Kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo anatarajiwa kupanda ulingoni Septemba 3, mwaka huu kupigana na Bondia wa Kimataifa wa Uingereza, Liam Mark Smith katika pambano la ubingwa wa
‘Super Welterweight’.
Kwa mujibu wa Mtandao wa Sky Sports Boxing, umeripoti kuwa pambano hilo litafanyika katika mji wa Liverpool nchini Uingereza kwenye Ukumbi wa M&S Bank Arena.
Historia ya bondia, Liam Mark Smith amezaliwa mwaka 1988 ambaye anapigana kwa mtindo wa ‘Orthodox’ kwa kutanguliza Mguu wa Kushoto mbele huku Mguu wa Kulia ukibaki nyuma, kama anavyopigana Bondia Hassan Mwakinyo.
Bingwa huyo wa zamani wa WBO, Liam Smith pambano lake la mwisho amepigana na bondia kutoka Marekani, Jessie Vargas kwenye ukumbi wa Madison Square Garden mjini New York nchini humo mapema mwaka huu.
Kwa ujumla Bondia huyo kutoka nchini Uingereza anaingia kucheza na Mwakinyo akiwa amepigana mapambano 35 huku akishinda mapambano 31 na ameshinda mapambano 18 kwa Knock Out (KO), amepoteza mapambano matatu na kupata suluhu pambano moja pekee.
Bondia Hassan Mwakinyo anakumbukwa kwa rekodi yake nzuri ya kumtwanga Bondia
Muingereza, Sam Eggington katika raundi ya pili, mjini Birmingham nchini Uingereza mwaka 2018, katika pambano la ubingwa wa ‘Super Welterweight’. Pia, Mwakinyo alimpiga Bondia kutoka Namibia, Julius Indongo mwezi Septemba, 2021 nchini Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...