NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amesema watumishi wa umma nchini wana deni kwa Rais Samia Suluhu Hassan la kufanya kazi kwa bidii, weledi na uadilifu kwani kwa kipindi cha Mwaka mmoja Rais ameonesha kujali maslahi yao.

Ndejembi ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara katika Halmashauri ya Babati Mji kwa ajili ya kuongea na watumishi wa umma na kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili.

" Watumishi wa Umma tuna deni kubwa kwa Rais Samia, ndani ya muda mfupi wa Uongozi wake kapandisha maslahi ya watumishi kwa kuongeza mshahara, kapandisha madaraja tumeona na posho pia zimeongezeka, hii inaonesha jinsi gani alivyo na mapenzi na sisi watumishi.

Ndani ya muda mfupi amelipa madeni ya watumishi mfano hapa Halmashauri ya Mji Babati Watumishi 358 wamelipwa malimbikizo ya mishahara yao ambayo ni zaidi ya Sh Milioni 371 ndani ya mwaka wa fedha 2021/22, watumishi 266 wamepanda madaraja kwahiyo mna deni kubwa kwa Rais na Watanzania katika kutoa huduma Bora," Amesema Ndejembi.

Ndejembi amesema litakua jambo la ajabu kuona watumishi wa umma wanaendekeza vitendo vya rushwa ilihali Serikali imewaboreshea maslahi yao na kwamba hawatosita kumchukulia hatua mtumishi yeyote ambaye atakosa uadilifu kazini.

" Niwaombe sana tufanye kazi kwa uadilifu, Serikali imeboresha haswa maslahi yenu ndani ya kipindi cha mwaka mmoja yamefanyika mambo makubwa kwa watumishi wa umma, itakua jambo la aibu kuona mtumishi wa umma anaendekeza vitendo vya rushwa mtu wa hivyo hatutomvumilia," Amesema Ndejembi.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...