UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA TAASISI YA UTAFITI WA MIFUGO TANZANIA (TALIRI)
Dodoma, Julai 26, 2022
Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kumteua Prof. Sebastian CHENYAMBUGA kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki (Mb), kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 8(1) na (2) (a - h) cha Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Na. 4 ya Mwaka 2012 amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 17 Julai, 2022 kama ifuatavyo:-
Prof. Joshua J. MALAGO ambaye ni Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro.
Prof. Esron D. KARIMURIBO ambaye ni Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro. Pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Veterinari Tanzania.
Dkt. Bugwesa Z. KATALE ambaye ni Mkurugenzi wa Uratibu na Uendelezaji wa Utafiti, Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dar es Salaam.
Dkt. Furaha P. MROSSO ambaye ni Meneja wa Utafiti wa Mazao,Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI), Wizara ya Kilimo, Dodoma.
Dkt. Angello J. MWILAWA ambaye ni Mkurugenzi wa Mafunzo, Utafiti na Huduma za Ugani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Mifugo), Dodoma.
Dkt. Stella BITANYI ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Dar es Salaam.
Bw. Yohana K. KUBINI ambaye ni Afisa Ushawishi na Utetezi, Chama cha Wasindika Maziwa Tanzania, Dar es Salaam.
Imetolewa na:-
Rehema H. Mbulalina
MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...