JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na kutengua uteuzi wa Dkt. Raphael Masunga Chegeni.
Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Suleiman Mzee alikuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP).
Uapisho utafanyika Ikulu Dar es Salaam, tarehe 1 Agosti, 2022.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...