Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa zawadi Nahodha wa Timu ya Taifa ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Gils) Noela Luhala kwa niaba ya Wachezaji wenzake kwenye hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Julai, 2022.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa, Katibu wa
Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi, Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu
nchini TFF Bw. Wallace Karia katika picha ya Pamoja na Timu ya Taifa ya
Wanawake wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Gils) kabla ya hafla ya
kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 17
(Serengeti Gils) pamoja na viongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na
Michezo katika hafla aliyowaandalia wachezaji wa Timu hiyo kuwapongeza
baada ya kufuzu kombe la Dunia la Vijana litakalofanyika nchini India.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...