Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

MKUU wa Mkoa  wa Pwani, Abubakar Kunenge ameagiza viongozi wa kata ya Kikongo  kushughulikia changamoto za migogoro ya ardhi na kusisitiza endapo atabaini kuna mtu mbabaishaji basi atashughulika naye.

Alitoa agizo Hilo wakati wa ziara ya kuzungumza na Wananchi wa  Kata ya Kikongo na kusikiliza changamoto iliyopo ya migogoro ya  ardhi kati ya wawekezaji na wanachi wa kata hiyo

Alieleza kuwa, Kata hiyo inadaiwa kuwa na changamoto na migogoro ya ardhi suala ambalo linapaswa kutafutiwa ufumbuzi.

Aidha, ameagiza shamba ambalo halina mgogoro  shamba namba  30/1 liendelezwe "kuna mashamba mawili moja lina mgogoro na lingine halina mgogoro kwanini ambalo halina  mgogoro lisiendelezwe." 
alisema Kunenge.
 
Mkuu huyo wa mkoa amesisitiza viongozi washughulikie haraka shamba lenye mgogoro ili wawekezaji waendelee na shughuli Yao.

"Baadhi ya viongozi acheni ubabaishaji,na nahimiza, suala la haki !!!"Mwenye haki apewe ama mwananchi ana haki apewe haki yake  na kama muekezaji  ana haki apewe  haki yake." alieleza Kunenge.

Vilevile,Ofisa Ardhi Grayson Gipson aliombwa  kutoa mrejesho uliotolewa kipindi cha Waziri  wa nyumba, Maendeleo na Makazi  William Lukuvi kwenye ziara yake aliyofanya  Julai 2021, ambapo alielekeza kuhusu mashamba mawili  yanayomilikiwa na Trans continental, la Kwanza ni 30/1 na la pili ni 30/2.

Ofisa ardhi huyo, alieleza  kuwa shamba namba 30/1 halina changamoto hivyo  kampuni ipo tayari kwa kufanya vipimo na kushughulikia shamba namba 30/1.

Alisema,  shamba namba 30/2 lina changamoto na  kampuni  ipo tayari kushughulikia shamba  namba moja tu ambalo   halina mgogoro.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...