Na Khadija Seif, Michuzi TV
WAKAZI wa Mtwara waanza Kuchagiza kuelekea pambano la "payback" linalotarajiwa kufanyika Julai 30 mwaka huu katika uwanja wa Majimaji Songea Mkoani Ruvuma.

Bondia wa Ngumi za kulipwa kutoka Mkoa wa Mtwara Osama Rabii amesema amejipanga vizuri kuelekea pambano la kitaifa "payback" dhidi ya mpinzani wake Doto Alai ambapo  Mtwara ni Miongoni mwa Mikoa ambayo imepewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao kwa Mabondia wakongwe na wanaochipukia katika pambano litakalompandisha Selemani Kidunda kutoka Tanzania na Erick Katompa kutoka Kongo kuwania Mkanda wa WBF.

Hata hivyo Rabii amehaidi kubadilisha mchezo wa Masumbwi katika Mkoa huo na ili waweze kupewa nafasi zaidi kitaifa na kutambulika Huku akimtaka mpinzani wake kufanya mazoezi ya kutosha sana kuelekea pambano hilo.

"Ninachomwambia mpinzani wangu ajipange kwa vigezo vyote kwa sababu ngumi siyo sanaa ya ngoma ila zinataka moyo, nitakwenda Songea kwa sababu ya kumpiga tena itakuwa ndani ya raundi ya pili ambayo hatoweza kumaliza."

Hata hivyo Mwalimu wa Mabondia wa Mkoa huo Mohammed Jumbe  amesema mabondia wote wako vizuri hivyo Mashabiki wajiandae kuona burudani nzuri na Mabondia wenye uwezo zaidi.

"Mtwara ni Mkoa ambao utaupeleka mchezo wa Masumbwi levo nyingine hivyo macho yote Songea kushuhudia uwezo huo na kuwaaminisha watu wa Mtwara na watanzania Kwa ujumla hivyo wasubiri ushindi huo."

Mabondia kutoka Mkoa wa Mtwara akiwemo Bondia wa Ngumi za kulipwa Osama Rabii  wakiendelea na mazoezi kuelekea pambano la "payback" julai 30 Songea Mkoani Ruvuma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...