Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

KAMATI  ya Utendaji ya Klabu ya Yanga SC imeridhia ombi la kutoongeza mkataba kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Senzo Hammilton Mazingiza baada ya kuwasilisha pendekezo hilo baada ya mkataba wake wa awali kuisha 31 Julai 2022.


Taarifa kutoka Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu hiyo imeeleza kuwa Senzo aliwasilisha ombi hilo lenye muktadha wa sababu za kifamilia ambayo amekuwa nayo mbali kwa kipindi cha miezi mitatu.


“Ombi la Senzo lilipokelewa na baada ya kujadiliwa, Kamati ya Utendaji ilikubali ombi hilo na kumteua, Wakili Simon Patrick kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa mpito (Interim Chief Executive Officer)”, taarifa imeeleza.


Klabu ya Yanga imemshukuru Senzo kwa utumishi wake ulio bora hasa katika mchango wake kwenye eneo la utawala na kumtakia ila la kheri.


Aidha, Kamati hiyo ya Utendaji imefanya kikao chake cha kwanza cha Kikatiba Julai 30, 2022 jijini Dar es Salaam chini ya Uenyekiti wa Rais wa Klabu, Mhandisi Hersi Said ili kujadili masuala mbalimbali ya Klabu hiyo likiwemo ombi la Senzo Mazingiza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...