Na Mwandishi wetu  - Dodoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Benki ya NBC kwa kuandaa  Marathoni ya “NBC Dodoma Marathoni,” kwa ajili ya kuchangisha fedha za  kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi nchini Tanzania. 

Akizungumza baada ya  mbio hizo Jijini Dodoma hii leo Julai 30,2022 Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa Serikali inathamini jitihada za sekta binafsi za kuungana mkono katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili jamii.

"Serikali inatambua kazi nzuri ya Mchango wa kijamii unaofanywa na Benki ya NBC kwa miaka mingi. Tunashukuru kwa ubunifu wa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na Chama cha Riadha Tanzania kuendeleza mbio hizi za marathoni zinazolenga kukusanya fedha za kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi nchini Tanzania"Amesema Majaliwa

Na kuongeza kuwa "Saratani ya shingo ya kizazi, ingawa inaongoza kwa kupoteza maisha ya wanawake nchini Tanzania, inaweza kuepukika na kutibika iwapo itagundulika mapema. Serikali inaunga mkono juhudi zote za kuongeza ufahamu wa wanawake na kuokoa maisha yao ya thamani,” Ameongeza

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi amesema kuwa Benki hiyo inafuraha kuandaa kipindi kingine cha mbio za NBC Bank Dodoma Marathon baada ya mafanikio mawili katika mbio zilizopita.

“Baada ya matoleo mawili yenye mafanikio ya mbio za Marathon hapa Dodoma, tunayo furaha kuandaa toleo hili la  tatu ambalo nalo limefanikiwa kwa kiasi kibwa na Pesa zote zilizopatikana, karibu TZS200 milioni, zitaelekezwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kusaidia mapambano ya wanawake dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi" Amesema Theobald Sabi

Na kuongeza kuwa "Ninayofuraha kutangaza kwamba katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, mbio za Marathoni zilikusanya zaidi ya TZS milioni 300 , ambazo zilisaidia kupima wanawake zaidi ya 9,000 wanawake, 550 kati yao waligundulika kuwa na saratani na kwa sasa wanaendelea na matibabu. 

Pia Sabi amewashukuru washiki wote  kwa uungwaji mkono kutoka pembe zote za bara la Afrika huku watu wakijumuika na Benk hiyo katika kazi hiyo adhimu.

Sabi ameongeza  kuwa  Benki ya NBC ina bahati ya kuweza kukusanya fedha ili kuokoa maisha na kuleta matumaini kwa familia mbalimbali hapa nchini.

Katika Marathoni ya mwaka huu imevutia zaidi ya washiriki 4,000 kutoka nchi 8 tofauti na katika mbio za umbali tofauti tofauti ikianzia na ile ya Kilomita 42,21 na 10 ambapo yafuatayo ni majina ya washindi katika mbio hizo kulinaga na kilomita;

1.KILOMETA 42.2 KWA UPANDE WA WANAUME

Namba moja imekwenda kwa Paul EYANAE,kutoka Kenya akitumia wasta wa masaa 02:14:45,namba mbilini  Erick CHEPKUMIA,kutoka Kenya akitumia wastani wa masaa 02:14:46,namba tatu ni Ezakiel KEMBOI,kutok Kenya akitumia watani wa masaa 02:15:04,4,3339,nafasi ya nne ikienda kwa Henry KICHANA,kutoka nchini Kenya akitumia wastani masaa 02:15:48,wakati Abraham TOO kutoka nchini Kenya ametumia watani wa masaa 02:16:40 akinyakua nafasi ya tano.

 KWA UPANDE WA WANAWAKE 

Mshindi wa kwanza ni Monica CHERUTO,kutoka nchini Kenya,akitumia wastani wa masaa 02:37:50 ,wakati nafasi ya pili i,ienda kwa Hellen MUSYOKA kutoka nchini Kenya akitumia wastani wa masa 02:37:59 huku Truphena CHEPCHIRCHIR kutoka nchini Kenya akiibuka na nafasi ya tatu 02:39:05,nafasi ya nne ikienda kwa Sara MAKERA,kutoka Tanzania akitumia wastani wa masaa 02:42:56, Wakati Peris JEPKORIR kutoka nchini Kenya akishika nafasi ya tano 

2.KILOMITA 21 UPANDE WA WANAUME

Nafasi ya kwanza imekwenda kwa Samwel MAILU, kutoka nchini Kenya akitumia wastani wa saa 01:02:05,huku nafasi ya pili ikienda kwa Wilflred KIRWA KIGEN,kutoka nchini Kenya akitumia wastani wa saa 01:02:14,Mshindi wa tatu ni Daniel Muindi MUTETI kutoka nchini Kenya akitumia wastani wa saa 1:02:59,nafasi ya nne imekwenda kwa Martin MUSYOKA kutoka nchini Kenya akitumia wastani wa saa 01:03:08, huku nafasi ya tano ikienda kwa kijana wa kitanzania Jonathan AKANKWASA akitumia wastani wa saa 01:03:09

KWA UPANDE WA WANAWAKE

Nafasi ya kwanza imechukuliwa na Agnes NGOLO kutoka nchini Kenya aliyetumia wastani wa saa 01:10:53, nafasi ya pili ikinyakuliwa na Sharon Jemutai KOSGEI akitumia wastani wa saa  01:11:45, Nafasi ya tatu ikinyakuliwa na Mercy Jerop KWAMBAI toka Kenya akitumia mda wa saa 01:14:34,nafasi ya nne ikienda kwa Edna Jerono KIMITEI toka nchini Kenya pia akitumia wastani wa saa 01:16:42 huku Harriet Agness AMURO kutoka nchini Uganda akishika nafasi ya tano akitumia muda wa saa 01:18:53.

3.KILOMITA 10 UPANDE WA WANAUME*

Katika mbio hizi nafasi zote tano zimechukukiwa na wanariadha kutoka Tanznania ambapo mshindi wa kwanza ni Jamal Waziri ALLY wa pili ni Decta BONIFACE,namba tatu ni Benard GEAY,namba nne imekwenda kwa Francis Damiano DAMAS na mshindi wa nne ni Nicodemus JOSEPH

KWA UPANDE WA WANAWAKE 

Katika mbio hizi nafasi zote tano zimechukukiwa na wanariadha kutoka Tanznania ambapo mshindi wa kwanza ni Anastasia DOLOMONGO namba mbili ni Aisha LUBUNA, huku namba tatu ikienda kwa Fatuma MNGA,namba nne ikinyakuliwa na Neema SANKA na nafasi ya tano ikienda kwa Neema KISUDA.

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ni moja ya benki zinazoongoza nchini Tanzania kwa kufanya kazi nchini kote kupitia mtandao mpana wa matawi, wakala-wakala, ATM, na Mashine za Uuzaji wa Pointi. Benki pia inafanya kazi kupitia majukwaa ya benki ya simu na mtandao.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akikabidhi hundi ya shilingi milioni 200 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road {ORCI}, Dk. Julius Mwaiselage (kulia) zilizopatikana kupitia NBC DODOMA MARATHON Jijini Dodoma hii leo Julai 31,2022 kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi nchini Tanzania.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akizungumza baada ya kukamilika kwa mbio za ( NBC DODOMA MARATHON) Jijini Dodoma hii leo Julai 31, 2022

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...