#Mapacha Waliotengenishwa waendelea vizuri Muhimbili

Na.Catherine Sungura,WAF-Dar es Salaama

Serikali kupitia Wizara ya afya imetenga billion 8 kusomesha watalaamu wa afya, ndani na nje ya nchi , katika fani mbalimbali za kibingwa ikiwemo upasuaji wa watoto.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi mara baada ya kuwajulia hali watoto mapacha (Rehema na Neema) waliokuwa wameungana na kufanikiwa kutengenishwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili mnamo Julai Mosi mwaka huu.

Prof. Makubi amesema kuwa fedha hizo zitawasaidia wataalamu wa afya ili kuweza kujiendeleza kwa ngazi ya kibingwa na ubingwa bobezi na kuwataka Watalaamu kujitokeza.

"Ili kuendelea kuboresha huduma za kibingwa nchini tumetenga bilioni 8 za kuwaendeleza wataalamu wetu ndani na nje ya nchi kwa fani mbalimbali ikiwemo upasuaji wa watoto".Amesema Prof. Makubi

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejenga mfumo bora wa vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya wagonjwa mahututi (ICU) kutoka ngazi ya Taifa hadi hospitali za Halmashauri.

Kwa upande wa watoto mapacha waliofanyiwa upasuaji wa kuwatengenisha Prof. Makubi amesema upasuaji huo wa kihistoria kwa watoto hao walioungana tumbo na kifua ni mfumo bora uliowekwa na Rais Samia Suluhu Hassan wa kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya kwa ngazi zote nchini.

"Rais Samia na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wanatoa pongezi kwa wataalamu wetu nchini wakishirikiana na wale wa chuo Kikuu cha Bahrain kwa kufanikisha upasuaji mkubwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili" Aliongeza

Aidha, Prof. Makubi amesema Mapacha hao wanaendelea vizuri chini ya uangalizi maalumu wa wataalamu wa hospitali ya Taifa Muhimbili.

Hata hivyo Prof. Makubi amewatia moyo na kuwashukuru wataalamu wa afya kwa huduma ya upasuaji na kusema kuwa Serikali itaendelea kuboresha mafunzo,vifaa, vifaa tiba pamoja na miundombinu katika eneo la upasuaji nchini.

Akizungumza kwa mara ya kwanza ,Mama wa pacha hao Bi.Amina Amos amesema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha wataalamu kufanikisha upasuaji wa pacha wake.

"Napenda kushukuru Taifa letu na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuwezesha kunitenganishia watoto wangu salama pamoja na Madaktari kutoka nje,nashukuru sana wauguzi hapa PIKU wamenilelea vema watoto wangu hadi sasa.

"Nimepata changamoto nyingi lakini sasa hivi ninafurahi kwa sababu napata kila mahitaji ya watoto, nimelelewa vizuri pamoja na watoto".

Katibu Mkuu Prof. Abel Makubi akiongea na Mama Mzazi wa Watoto Mapacha (Rehema na Neema) waliokuwa wameungana na kufanikiwa kutengenishwa mara baada ya kuwatembelea katika hospitali ya Taifa Muhimbili.Mapacha hao wanaendelea vizuri




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...