Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali katika shamra shamra za maadhimisho ya mwaka Mpya wa Kiislamu (1444 Hjr)yaliofanyika katika Mnara wa kumbukumbu Kisonge Zanzibar.



Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa akitoa Damu ikiwa ni Ishara ya uzinduzi wa Maadhimisho ya mwaka Mpya wa Kiislamu (1444 Hjr)kwa Watu mbali mbali kujitokeza kuchangia Damu katika Mnara wa kumbukumbu Kisonge Zanzibar.



Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali akitoa Damu katika Hafla ya Uzinduzi wa Maadhimisho ya mwaka Mpya wa Kiislamu (1444 Hjr)kwa Watu mbali mbali kujitokeza kuchangia Damu katika Mnara wa kumbukumbu Kisonge Zanzibar.



Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Sheikh Khalid Ali Mfaume akitoa Damu katika Hafla ya Uzinduzi wa Maadhimisho ya mwaka Mpya wa Kiislamu (1444 Hjr)kwa Watu mbali mbali kujitokeza kuchangia Damu katika Mnara wa kumbukumbu Kisonge Zanzibar.



Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maadhimisho ya mwaka Mpya wa Kiislamu (1444 Hjr)ambapo Watu mbali mbali kujitokeza kuchangia Damu katika Mnara wa kumbukumbu Kisonge Zanzibar.



Baadhi ya wananchi mbalimbali waliojitokeza kuchangia Damu katika Shamra shamra za Uzinduzi wa Maadhimisho ya mwaka Mpya wa Kiislamu (1444 Hjr)kwa Watu mbali mbali kujitokeza kuchangia Damu katika Mnara wa kumbukumbu Kisonge Zanzibar.





Misururu ya watu mbalimbali waliojitokeza kuchangia Damu katika Shamra shamra za Uzinduzi wa Maadhimisho ya mwaka Mpya wa Kiislamu (1444 Hjr)kwa Watu mbali mbali kujitokeza kuchangia Damu katika Mnara wa kumbukumbu Kisonge Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

………………………………………

Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana Mustafa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha wa watu katika jamii

Akizungumza mara baada ya kuchangia damu hiyo katika Mnara wa Kumbukumbu Kisonge ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha mwaka mpya wa kiislamu, amesema kuchangia damu ni muhimu kwani taifa linahitaji mkubwa hivyo ni vyema jamii ikahamasika katika zoezi hilo

Amesema kumekuwa na upungufu wa damu katika baadhi ya vituo vya matibabu jambo ambalo linahatarisha maisha ya watu kufanya hivyo kutasaidia kuokoa uhai wananchi.

Mkuu huyo ameishukuru Ofisi ya Mufti kwa kuaanda kufanya jambo jema la kuimarisha afya za wagonjwa na kuweka kumbukumbu za mwaka mpya wa kiislamu wenye kuleta manufaa kwa jamii.

Nae Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali amesema kuwa wameamua kusheherekea mwaka mpya wa kiislamu kwa kuchangia damu ili kuisaidia jamii kwani kuna uhitaji mkubwa wa damu katika vituo vya afya.

Amefahamisha kuwa zoezi hilo ni la kwanza ambalo limeanzia katika Mkoa wa Mjini Magharibi na litakuwa endelevu katika Mikoa yote ili waislamu waweze kufahamu miaka ya kiislamu na kuwataka waislamu kuwa tayari kufanya zoezi hilo ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu.

Nao wananchi wamesema kuwa kitendo cha kuchangia damu kitasaidia wagojwa wenye mahitaji ni vyema waislamu kuunga mkono Ofisi hiyo kwa uwamuzi wake wa kuanzisha jambo hilo.

Wameeleza kuwa kuadhimisha mwaka mpya wa kiislamu isiishie hapo bali iwe ni njia ya kujitathmini kwa kuazimia kufanya mabo mema ya kwani kufanya jambo zuri ni ibada kwa waislamu na jamii kwa ujumla.

“Tusisheherekee tu kuingia mwaka mpaya wa kiislamu bali pia tuangalie nini tumefanya tulikotoka na tunakokwenda , jambo gani jema ambalo tumefanya kwa ajili ya kesho tunatakiwa kila ukiingia mwaka tuzidishe ibada kwa wingi”,walisema wachangiaji hao.

Hata hivyo wameishauri jamii kujitokeza kuchangia kwa ajili ya kuwasaidia wale ambao wanahitaji kwani kufanya hivyo ni ibada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...