Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye
(wa pili kushoto) akimkabidhi Ripoti ya Utafiti wa Gesi Ukaa, Mkurugenzi
Mtendaji wa Simbagas, David Ndelwa (wa pili kulia) kwa ajili ya kampuni
hiyo kuanza uchimbaji wa gesi hiyo mkoani Mbeya, hafla ya makabidhiano
ilifanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam . Kushoto ni Mkuu wa Mkoa
wa Mbeya Juma Homera na kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Simba, Farid
Nahdi(kushoto) ni (Kushoto) ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi
(TPSF), Angelina Ngalula .
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye
(wa pili kushoto) akimkabidhi Ripoti ya Utafiti wa Gesi Ukaa, Mkurugenzi
Mtendaji wa Simbagas, David Ndelwa (wa pili kulia) kwa ajili ya kampuni
hiyo kuanza uchimbaji wa gesi hiyo mkoani Mbeya, hafla ya makabidhiano
ilifanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ,wa pili kutoka kulia ni
Mkuu wa kitivo cha Jiolojia na Madini wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Dkt Elisante Mshiu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kushoto ni Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera.
Mkurugenzi Mtendaji wa Simbagas, David Ndelwa, akizungumza wakati wa hafla

Baadhi ya viongozi wa Serikali kutoka mkoani Mbeya wageni waalikwa wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo.
Kampuni
ya Kitanzania ya Simba Gas, inajiandaa na uchimbaji wa gesi ya ukaa
(Carbon dioxide) huku ikilenga kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya bidhaa
hiyo katika soko la ndani na nje.
Uchimbaji utaanza baada ya kupata vibali vyote vya udhibiti kutoka katika taasisi zote zinazohusika.
Haya
yanajiri wakati kampuni hiyo ikipata uhakika wa upatikanaji wa gesi ya
ukaa katika eneo la Kata ya Suma lililopo Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa
Mbeya baada ya zoezi la utafiti wa miezi miwili lililofanywa na
wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Simba
Gas - ambayo ilisajiliwa mwaka 2021 kama sehemu ya kundi la makampuni
ya Simba ikijikita katika kuchimba na kuuza gesi ya ukaa imepokea
matokeo ya utafiti kutoka kitivo cha jiologia na Madini cha Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam wakati wa hafla iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa
sekta ya Nishati na Madini ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya, Mh. Juma Zuberi Homera.
Gesi
ya Ukaa hutumika katika utengenezaji wa vinywaji vyenye gesi, Pia
hutumiwa kama kipoozo katika vizima moto kwa kuingizwa katika vifaa vya
uokoaji, uchomelea vyuma katika miradi mikubwa, utengenezaji wa barafu
kavu (dry ice) zinazotumika kupozea vinjwaji , ulipuaji wa makaa ya
mawe, utengenezaji wa vifaa vya mpira na plastiki, ukuzaji wa mimea
katika vitalu nyumba na pia kupunguza nguvu za wanyama kabla ya
kuchinjwa.
Akiongea
wakati wa hafla ya kupokea ripoti ya utafiti, Mkurugenzi wa kampuni
Simba Gas ndugu David Ndelwa, alisema soko la gesi ya ukaa linakua kwa
kasi kubwa ndani na nje ya nchi. "Kwa sasa, mahitaji ya gesi ukaa katika
soko la ndani yanafikia tani 1,060 kwa wiki na tunao upungufu wa tani
360 kwa wiki,” alisema.
Vile vile, mahitaji ya soko la mauzo ya nje la gesi ya ukaa kwa sasa ni takribani tani 2,000 ambapo upungufu ni tani 1,460.
"Inakadiriwa
kuwa hadi sasa, soko la kimataifa la gesi ukaa linafikia thamani ya
dola bilioni 10.36. Kampuni yetu imejiandaa vya kutosha na itawekeza kwa
kiasi kikubwa ili kuhakikisha kuwa tunatumia rasilimali tulizo nazo ili
kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi,” alisema David Ndelwa
David
Ndelwa alisema Simba Gas, imefanya utafiti na kuona soko kubwa la gesi
ukaa katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Congo, Malawi, Msumbiji, Afrika
Kusini, Botswana, Angola, Sudan Kusini, Rwanda na Namibia pamoja na
nchi nyinginezo.
“tunatambua
kwa kusafirisha gesi yetu nje ya nchi, tutaleta fedha za kigeni nchini.
Pia tutazalisha nafasi za ajira za moja kwa moja 150 na zingine 300 za
muda maalum” alisema.
Hata
hivyo alibainisha kuwa tafiti zaidi zitalazimika kufanyika ili kukidhi
matakwa ya kimataifa ya uvunaji wa bidhaa hiyo na ameiomba Serikali
kuendelea kuweka mazingira mazuri yatakayovutia ufadhili zaidi wa
shughuli hizo.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh. Juma Zuberi Homera, alisema
Serikali, inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, inajitahidi
kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia uwekezaji katika sekta ya
nishati na viwanda miongoni mwa mambo mengine.
Aliipongeza
Simba Gas kwa kuwekeza Mbeya, na kubainisha kuwa kwa kufanya hivyo,
kampuni hiyo itakuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha azma ya
serikali ya kukuza sekta ya uwekezaji na kuisaidia nchi kukuza uchumi
wake.
"Mradi
huu utakapoanza rasmi, utazalisha ajira, kuongeza mapato ya serikali za
mitaa na kusaidia jamii kupitia mipango ya uwajibikaji kwa jamii,"
alisema, akibainisha kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono uwekezaji
huo.
Naye
Mkuu wa kitivo cha Jiolojia na Madini wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Dkt Elisante Mshiu alisema anawashukuru kampuni ya Simba Gas kwa
kuwaamini wataalamu wa ndani ambao wamejikita kuleta ukombozi na mageuzi
makubwa ya kufanya tafiti za kimkakati na kuhakikisha taifa linanufaika
na lasilimali zake.
Simba
gesi wamedhubutu kufanya tafiti katika uchimbaji wa gesi ukaa,
tunaamini watafungua fursa nyingi pia kwa vijana wetu ambao
tunawazalisha wakiwa wamebobea katika kuendesha mitambo ya gesi na
itafungua milango ya ajira kwa vijana wetu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...