Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), Fransis Lupokela, akionesha baadhi ya michoro wakati wa maonesho ya Kimataifa ya kibiashara ya 46 katika Viwanja vya J.K. Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam leo Julai 4, 2022.

Mhandisi Mitambo ya kuchakata gesi Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), Herman Edward akizungmza na wananchi waliotembelea banda la Shirika hilo katika Viwanja vya savbasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), Fransis Lupokela,akizungumza wakati wa maonesho ya Kimataifa ya kibiashara ya 46 katika Viwanja vya J.K. Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam leo Julai 4, 2022.

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), limesema linaendelea kuongeza upatikanaji wa gesi katika vyanzo mbalimbali ambavyo watafiti wapo kazini kutafuta gesi na mafuta nchini.

Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), Fransis Lupokela, amesema hayo wakati wa maonesho ya Kimataifa ya kibiashara ya 46 katika Viwanja vya J.K. Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam leo Julai 4, 2022, amesema kuwa kuwa Shirika hilo limefanikiwa kugundua gesi katika maeneo ya mbalimbali, shirika linaendelea katika shughuli za utafiti wa mafuta na Gesi katika mkondo wa Juu wa Kati na wachini.

Amesema kuwa tayari kuna Viwanda 48 vinavyotumia gesi asilia, nyumba 1500 na Hoteli ya Serena, tasisi za mbili za serikali ambazo ni Gereza la Mtwara na la Keko pamoja na shule nne na Magari 1400.

Lupokela amesema katika Mkondo wa juu shirika linamiradi ya kimkakati ya ambayo ni Eyasi ni mradi ambao wanatafuta mafuta na gesi katika ziwa Eyasi, linalogusa mikoa ya Singida, Arusha, Tabora na Simiyu.

Amesema kitulu hicho cha Eyasi kinafanana sifa zake kijiolojia na kitalu cha Uganda na Kenya ambapo wamegundua mafuta hivyo inawapa hamasa kuwa wagundua Mafuta na gesi katika Maeneo hayo.

Akizungumzia mradi Mwingine Lupokela amesema katika Mradi wa Mnazi Bay Kaskazini (North) wanaendelea kufanya tafiti za kugundua gesi pamoja na mradi wa Songosongo (west) Magharibi

Amesema nchi mpaka sasa inamiundombinu Mitatu ya gesi asilia ambayo ni Songas, MNP (Mkomanzi National Park) ambao unaishia Mtwara na Miundombinu ya taifa ya gesi asilia (LNG)(Mradi wa Gesi asilia na Gesi Asilia iliyosindikwa), ambalo ni bomba kubwa la gesi asilia ambalo linasaidia kuzalisha umeme kwa asilimia 62 ambao upo kwenye gridi ya Taifa unazalishwa kutokana na gesi asilia.

Amesema kuwa hii ni njia mojawapo ya kuiondolea serikali gharama za kuzalisha umeme nchini.

"Katika maonesho ya sabasaba tunaonesha Moja kwa moja kuwa wanachi anajua kuwa matumizi ya gesi asilia yanakuwa na kuonesha namna gani viwanda vinatumia gesi asilia Pamoja na Mahoteli." Amesema Lupokela

Katika kuhakikisha gesi asilia inapatikana majumbani amesema kuwa shirika la TPDC linaendelea kufanya tafiti za kuongeza upatikanaji wa gesi tayari serikali imeruhusu Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kushirikiana na TPDC wanafadhili ili kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi.

Ili kuhakikisha kwamba gesi asilia inafika maeneo ya mikoani tayari wamejipanga kusambaza kwa njia tatu ambazo zinaweza kufikisha gesi hiyo kwa njia ya mabomba na usindikaji wa gesi katika maeneo husika.

Amesema wamehafanya mawasiliano na chuo kikuu Cha Dar es Salaam kuomba eneo kwaajili ya kusindika gesi asilia ili kuweza kuhudumia vituo vidogo vidogo vingi zaidi.

Amesema pia kunamradi wa bomba la Mafuta kutoka Uganda Hoima mpaka Chogoleani Tanga ni moja ya miradi ambayo TPDC inafanya kwa niaba ya serikali na unapaisha Taifa kuwa ni kituo cha Mafuta.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...