Na Mwandishi Wetu

Abuja, Nigeria

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Nigeria na Uwakilishi wa nchi nyingine 14 za Afrika Magharibi, ulifanya maadhimisho ya siku ya Kiswahili Duniani nchini hapa.

Maadhimisho hayo yaliyofanyika sambamba na maonesho ya Filamu ya Tanzania the Royal Tour, ni kutokana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni, (United Nations Education, Scientific and Cultural Organization -UNESCO), Novemba 23, 2021 wakati wa Mkutano wa 41 wa nchi Wanachama walipitisha Julai 7, kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili Duniani.

Uamuzi huo ulifikiwa kutokana na Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha 10 zinazozungumzwa zaidi ulimwenguni.

Maadhimisho hayo yaliyofanyika Jijini Abuja, yalihudhulia na Jumuiya ya Wanadiplomasia (kutoka Balozi za Afrika Kusini, Rwanda, Uganda, Burundi, Kenya, Kongo-DRC, Bulgaria, Palestine, Burkina Faso, Cuba, Mali, Guinea, Poland, Senegal), ambapo Mwakilishi wa UNESCO nchini Nigeria, Asasi za kiraia (kama vile women in Business and Tourism, Women Arise, wafanyabiashara, maofisa kutoka taasisi za Serikali ya Nigeria kama vile Voice of Nigeria, Nigerian Export Promotion Council, taasisi za elimu (kama vile Chuo Kikuu cha Ghana, Legon, Chuo Kikuu cha Port Harcourt, Chuo Kikuu cha Ibadan, Taasisi ya SOS ya Ghana): Diaspora Afrika Mashariki na vyombo vya habari (kama vile Voice of Nigeria, Nigeria Television Authority, na wadau wengine wa karibu wa Ubalozi.

Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Botswana nchini Nigeria, Pule Mphothwe.

Pamoja na mambo mengine, maadhimisho yamliambatana na mdahalo wa wazi kuhusu ambao ulijadili kuhusu mchango wa Kiswahili katika ukombozi wa Bara la Afrika; Umuhimu wa Lugha katika ujenzi wa taifa; nafasi ya kimkakati ya Lugha ya Kiswahili katika kufikia malengo ya Eneo Huru la Biashara Barani Africa, AfCFTA; changamoto na uzoefu wa kufundisha Lugha ya Kiswahili katika taasisi za elimu Afrika Magharibi na changamoto zinazovikabili vyombo ya habari katika kutangaza idhaa za Kiswahili Afika Magharabi.

Wakati wa maadhimisho hayo, Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria, uliwapatia vyeti vya kushiriki mafunzo ya awali wafanyakazi 10 wa Nigerian Export Promotion Council, NEPC.

Wanafunzi hao waliweza kushiriki mafunzo hayo kikamilifu, mbali na changamoto na wingi wa majukumu mengine ya kikazi.

Mafunzo hayo yaliyodumu kwa takribani miezi sita, yaliendeshwa na Ubalozi kwa Kushirkiana na NEPC kuanzia Novemba 2021, ambapo darasa hilo linakusudia kuendelea na mafunzo ngazi ya juu.

Sambamba na maadhimisho hayo, ubalozi ulitumia fursa hiyo kuwaonesha washiriki Filamu ya Tanzania the Royal Tour, ikiwa ni moja ya mikakati wa kutangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania Bara na Zanzibar.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...