Na Jane Edward,Arusha


Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere amesema Tanzania itafikia lengo la kuwa na uhakika wa usalama wa chakula kwa kusimamia sera na miongozo ya uzalishaji wa mbegu bora zitakazotosheleza mahitaji ya ndani na kuondokana na dhana ya kutegemea kuagiza pembejeo za kilimo kutoka nje ya nchi.

Makongoro ametoa rai hiyo jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa kongamano la wadau wa mbegu waliokutana kwaajili ya kujadili ufanisi katika ushirikiano na serikali kwenye kuboresha mazingira ya kisera na udhibiti kwenye sekta ya mbegu.

Amesema kuwa sera na miongozo ya nchi katika sekta ya kilimo hususani mbegu inatakiwa isimamiwe imara ili kuwa na mbegu bora ambayo itatoa mazao bora yatakayosaidia kukuza uchumi wan chi pamoja na kipato cha mkulima.

‘’Ni wakati sasa wa wazalishaji wa mbegu kujikita kutengeneza mbegu bora ili jamii na nchi za jirani ziweze kujua kuwa mbegu bora zipo Tanzania’’Alisema

Amesema kuwa katika suala la kilimo siasa inabidi kuondoka ili kuwezesha kilimo kuwa cha kibiashara na kunufaisha jamii ya watanzania na wakulima wenyewe ambao wanapambana kuhakikisha wanapata mazao bora yatakayokuwa na tija.

Awali akielezea kuhusu muelekeo wa Tanzania kwenye sekta ya mbegu afisa mtendaji mkuu mpango wa kukuza kilimo ukanda wa kusini mwa Tanzania SAGCOT Geofrey Kirenga amesema kwa kutekeleza dhana ya ushirikishwaji Tanzania imekuwa moja ya nchi za mfano wa kuigwa.

Aidha amesema kuwa wakulima wasipotunza udongo kwa uhakika kupata mbegu bora itakuwa historia kutokana na wakulima kupaswa kupata elimu kutoka kwa maafisa ugani ambapo wakulima na maofisa ugani kufanya kazi kwa pamoja ili kuwa na mbegu bora.

Taasisi yenye jukumu la kusimamia makampuni ya uzalishaji na uagizaji wa mbegu nchini [TASTA] Bob Shuma ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hilo wanasema ushirikiano wa serikali katika sekta hiyo ya mbegu umekuwa wa mafanikio na matokeo chanya.

Amebainisha kuwa Tasta kwa sasa imekuwa ya pili barani Afrika kwa kusimamia sekta ya mbegu ikifatiwa na nyingine iliyoko south Afrika ambapo anasema hiyo yote imetokana na kufanya kazi na serikali kwa karibu pamoja na wadau wa mbegu na hiyo ndiyo siri ya mafanikio hayo.

Amesema misingi imara inapaswa kuboreshwa kwa kushirikiana na serikali ili kuweza kuwezesha vizazi vijavyo kujivunia uwepo wa TASTA kwa kuweza kutekeleza majukumu yake kwa kuitaka serikali kuendelea kufanya kazi na sekta binafsi ili kuweza kufika mbali.


Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere akikata utepe wa kuzindua mpango mkakati wa Tasta.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara akikabidhi mpango mkakati wa Tasta kwa mdau wa mbegu.
Washiriki wa kongamano la wadau wa mbegu wakifatilia mijadala inayojadiliwa kuhusu mbegu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...