Na Innocent Melleck
Mwanariadha Alphonse Felix Simbu ameshinda nafasi ya pili katika mashindano ya mbio za marathoni ya Jumuiya ya Madola yanayoendelea nchini Uingereza.
Ushindi huo ni mfululizo na mafanikio yaliyopatikana katika miaka ya hivi karibuni kutokana na utekelezwaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025.
Ilani ya CCM inaielekeza Serikali ya Rais Samia kuimarisha na kulinda miundombinu ya michezo ya wilaya, mikoa na Taifa sambamba na kuanzisha vituo viwili vya michezo (sports academy) vya Serikali pamoja na kuendelea kuviimarisha vituo vya Dole na JKU na vingine kwa kushirikiana na taasisi binafsi ili kuendeleza uibuaji wa vipaji.
Aidha, inaielekeza Serikali kuhifadhi miundombinu ya michezo katika skuli,mitaani na maeneo ya fukweni pamoja na kuwatambua na kuwawezesha wanamichezo wenye ulemavu kupata fursa na haki ya kushiriki katika mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Pamoja na hayo, inaitaka Serikali kuhamasisha vyama vya michezo kufanya jitihada za kupata uwanachama wa kudumu katika mashirikisho ya michezo kikanda, kitaifa na kimataifa na kusimaimia vyema vilabu kushiriki kikamilifu
katika mashindano ya kitaifa, kikanda na kimataifa sambamba na kuhamasisha jamii kushiriki katika mazoezi ya viungo na michezo mtu mmoja mmoja au vikundi na kuendeleza Tamasha la Mazoezi ya Viungo la tarehe mosi Januari kila mwaka.
Sambamba na hayo, CCM inaielekeza Serikali iliyopo madarakani
kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa michezo katika skuli, vikosi,
wizara, mitaa na jamii kwa ujumla kwa kushirikiana na vyama
husika pamoja nakuhamasisha jamii kushiriki katika michezo yote ya kisasa na asili ikiwemo michezo ya bao, karata na resi za ngalawa.
Home
MICHEZO
Ushindi wa Simbu Unatokana na Utekelezaji wa Maelekezo Yaliyopo Kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...