NA BALTAZAR MASHAKA, NYAMAGANA

WAUMINI mbalimbali wa Dini ya Kiislamu wamechangia fedha na vifaa vya miradi ya ujenzi wa vituo vya afya vyenye thamani sh. milioni 8.9.

Vifaa hivyo zikiwemo fedh tasilimu sh.580,000 vilichangia jana baada ya sala ya Eid El-Hadha iliyofanyika katika Uwanja wa Nyamagana.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Juma Mvanga alisema miradi hiyo yenye majengo 12 kila kituo bado wako nyuma ingawa itakuwa na tija kwa afya za wananchi na jamii,hivyo wasichoke kuchangia ikamilike na kutoa huduma lakini bado .

“Nikupongeze Sheikhe Hasani Kakebe kwa maono na ubunifu huu wa ujenzi wa vituo vya afya,miradi hiyo italeta tija.Nafahamu watu wanavyotaabika huko kiafya,lakini tunaonekana tumechoka kabla ya kufika mwisho wa safari,” alisema na kuchangia matofali 1000.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Seleman Sekiete, alisema anaunga mkono ujenzi wa miradi hiyo kwa kuchangia mifuko 100 ya saruji, kwamba waislamu wana dhima ya kujijengea miundombinu ya kuihudumia jamii ikiwemo miradi hiyo ya afya na itakapokamilika itakuwa na tija kwa wananchi,jamii na waislamu katika masuala la afya.

Alitumia fursa hiyo kumpogeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa upendo, maono na dhamira yake ya kuwahudumia wananchi na kumwombea dua huku akiwataka wananchi na waislamu kujitokeza kushiriki kuhesabiwa siku ya sensa ifikapo Agosti 23, mwaka huu.

Pia Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi alisema kutokana na moja ya miradi hiyo kutekelezwa wilayni humo atashiriki katika harambee kubwa itakayofanyia Julai 30, mwaka huu ambapo jana alichangia mifuko 100 ya saruji.

Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Ramadhan Ng’anzi ambaye alichangia matofali 1000, alisema bila afya bora na imara ni vigumu kufanya jambo lolote la maendeleo.

Wengine waliochangia ni pamona na Othman Othman,matofali 1000,Mwenyekiti wa CCM Tawi la Butimba, Khalfan Kahabuka,matofali 100,dereva aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamis alichangia matofali 100 huku mmumini mwingine akiahidi tripu tatu za mchanga.

Akizungumzia miradi hiyo ya afya, Sheikhe Hasani Kabeke alisema iwe mvua iwe jua,afe kipa ama beki, lazima ikamilike na kuwataka waislamu kuondokana na unyonge na udhalili, wajitoe kuchangia maendeleo yao.

"Tunataka kuondoa unyonge wa waislamu kwa kuwa na miradi ya kuisaidia serikali kuhudumia jamii katika sekta ya afya,pia tuache kulalamika tumeachwa nyuma kwa maendeleo,"alisema.

Sheikhe huyo wa mkoa alisema njia pekee ya kuondoa malalamiko hayo ni kusomesha watoto wapate elimu bora na hatimaye waje kuwahudumia kwa sababu serikali haiwezi kumpa ajira mtu asiye na elimu na ambaye hajasoma.ssss    
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiswali sala ya Eid El-Hadha leo katika Uwanja wa Nyamagana wakiongozwa na Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikhe Hasani Kabeke.Picha na Baltazar Mashaka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...