Na Karama Kenyunko Michuzi TV
KAMPUNI ya simu ya mkono Vodacom imekabidhi vifaa na samani kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Bethsaida inayotoa elimu kwa watoto yatima wa kike jijini Dar es Salaam vitavyowasaidia katika masomo yao na kupelekea kuongezeka kwa ufaulu.

Vifaa na zamani vilivyotolewa ni viti 100, vitabu Zaidi ya 380 pamoja na vifaa 20 vya kuzalisha umeme wa jua (SOLA)

Akiongea wakati wa makabidhiano, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania, Vivienne Penessis amesema, elimu ndio msingi pekee ambao unampatia mtu kianzio cha kujenga miasha bora maishani hivyo basi zawadi hiyo ni kwa ajili ya watoto hao yatima ambao tegemeo lao kubwa ni elimu pekee.

Amesema, shule hiyo imechaguliwa na wafanyakazi wa Vodacom kupatiwa msaada huo kwa kuwa ni moja ya shule chache zinazotoa elimu ya sekondari kwa Watoto yatima wa kike nchini.

Mkurugenzi hiyo ameeleza kuwa, ni Imani yake kuwa msaada huo utatumika ipasavyo kwani kampuni ya Vodacom imeijiridhisha juu ya utaalam na moyo wa kujitoa wa wafanyakazi wa shule ya Bethsaida.

Msaada huu unaendana na malengo ya Vodacom Tanzania kuongeza ujumuishwaji katika elimu. Hivi karibuni, kampuni ya Vodacom ilizindua mpango wa kupanua wigo wa mfumo wa E-Fahamu kufikia nchi nzima. E-Fahamu ni huduma inayotoa mawaidha ya elimu yenye viwango vya kimataifa na vyenye kukidhi miongozo ya serikali juu ya elimu.
Kuhusu Vodacom Tanzania Foundation.

Kwa upande wake, Mkuu wa shule hiyo, Hollynes Kwayu ameishukuru Vodacom kwa msaada huo mkubwa waliowapatia kwani utaongeza ari ya wanafunzi kusoma na hata walimu kufundisha kitendo kitakachopelekea kuongezeka kwa ufaulu shuleni hapo.

Amesema, kwa sasa wanawatoto 120, mankwamba walikuwa na changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa viti kutokana na vingi walivyokuwa navyo kuwa vimevunjika.

Amesema, walikwishaomba misaada katika sehemu mbali bila ya mafanikio mpaka leo hii Vodacom walipojitokeza na kufufua ndoto za wanafunzi za kusoma nyakati zote hata wakati wa giza..

"Ninaamini, vifaa hivi yaani, Viti, vitabu na Sola tulizopatiwa leo vinakwenda kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wetu, kwani mwanzoni kitabu kimoja kilikuwa kinatumiwa na wanafunzi watano lakini baada ya kupokea msaada huu, kitabu kimoja kitakuwa kinatumiwa na wanafunzi wawili, huku Sola nazo zikiwasaidia kusoma mpaka usiku (Prep)". amesema Mwalimu Kwayu

Amesema hata walimu watakuwa na amani ya kufundisha maana wakati mwingine walimu walikuwa wanaondoka kwa sababu ya mazingira magumu ya kufundishia.

Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, Easter Gadi Ameishukuru Vodacom na kusema kuwa, "tunashukuru sana kwa msaada wenu mliotutolea katika shule yetu, mmetusaidia kwa upande mkubwa hasa hasa katika masomo yetu, mfano sola zitaweza kutusaidia mpaka usiku tukitaka kujisomea wenyewe hasa tukiwa tunajiandaa na mitihani, viti hivi vitatusaidia tukae kwa raha na kuweza kuelewa zaidi na vitabu navyo nitatusaidia katika masomo yetu.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis(katikati) akikabidhi baadhi ya vitabu kwa mkuu wa shule ya sekondari ya watoto yatima ya wasichana, Bethsaida iliyoko Mpiji Magoe jijini Dar es Salaam, Hollness Moshi (kushoto) ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom kwa shule hiyo, wafanyakazi hao wametoa viti 100, meza 100, vifaa vya kuzalisha umeme jua (solar power) 20 na vitabu 388. Kulia ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa sheria, Agapinus Tax na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis akikata utepe kuzindua rasmi vifaa vilivyotolewa na wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania kwa shule ya sekondari ya watoto yatima ya Bethsaida iliyoko Mpiji Magoe jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa sheria, Agapinus Tax , Mkuu wa shule hiyo, Hollness Moshi (wanne kulia), Mlezi wa shule, Michael Machali (kulia) na Mwakilishi wa bodi ya shule, Said Ngonyani (watatu kushoto)
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis akizungumza kwenye hafla hiyo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...