Na Jane Edward, Arusha

Ofisi ya Waziri Mkuu katika kutekeleza Sheria ya usimamizi wa maafa imeànza kuimarisha uratibu wa shughuli za udhibiti wa maafa kwa kuhakikisha uwepo wa mfumo thabiti katika ngazi Zote

Katika ufunguzi wa jukwaa la Wadau wa udhibiti wa maafa kwa ajili ya kujadili na kudhibitisha mpango wa Taifa wa kujiandaa na kukabiliana na maafa na mkakati wa mawasiliano wakati wa dharura uliowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya maafa jijini Arusha

Mkurugenzi idara ya menejiment ya maafa kutoka Ofisi ya waziri Mkuu Meja Jenerali Michael Mumanga,anasema lengo la jukwaa hili Ni kutoa fursa kwa Wadau kutoa maoni yao kwa lengo la kuboresha na kuthibitisha mpango ulioandaliwa

Jenerali Mumanga anasema kutokana na kuongezeka kwa matukio ya majanga ambayo yamekuwa yakisababisha maafa,serikali kwa kushirikiana na wadau wameona Ni muhimu kuwa na mipango mikakati yenye lengo la kujiandaa na kupunguza vihatarishi vya maafa

"Mipango hii mikakati ni kuhakikisha kuwa pindi maafa yanapotokea ni namna gani nchi itawajibika katika kutatua au kupunguza maafa hayo" Alisema jenerali

Kwa upande wao Wadau wa maendeleo wanasema kukutana kwa wataalam Hawa Kuna lengo la kupitia na kujadili namna ya kupunguza athari za majanga

Mpango huu wa Taifa wa kujiandaa na kukabiliana na maafa ulianza mwaka 2012 ukizishirikisha Taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali.

Jenerali Michael Mumanga Akizungumza na wadau wa maafa jijini Arusha.
Wadau wa maafa wakiwa katika makundi kujadili namna ya kukabiliana na maafa pindi yanapotokea.
Mkuu wa uendeshaji UNDP, Jeremiah Malengo ambao ndiyo waratibu wa vikao kazi hivyo vya kujadili Maafa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...