Benki ya Akiba imetoa wito kwa wananchi kutembelea banda lao katika maonesho ya 46 ya kimataifa ya biashara maarufu kama sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam, ili kupata huduma kutoka katika benki hiyo.

Meneja Msaidizi wa Masoko, Innocent Ishengoma ambaye alikuwa kwenye banda lao, amesema kuwa benki hiyo imejipanga vizuri kutoa elimu na huduma mbalimbali kama vile, kufungua akaunti, mikopo pamoja na bima

"Tumekuja na huduma mbalimbali za kidigitali mfano Akiba Mobile ambapo mteja anaweza tumia huduma yetu ya Akiba mobile kujipatia huduma za kibenki popote pale alipo, masaa 24, siku saba za wiki"

"Lakini pia benki ya Akiba tunao mawakala wetu takribani 1200 ambao wamesambaa Tanzania nzima kwa ajili ya kutoa huduma.Utakapo tembelea banda letu utapata huduma ya kufungua akaunti papo kwa papo na maelezo mengine kuhusiana na huduma mbalimbali mathalani Mikopo na bima.

Pia Ishengoma ameongeza kusema kuwa katika maonesho ya mwaka huu ya 46 wamekuja na huduma mpya za bima, bima za maisha na bima kwa ajili ya vitu mbalimbali kama vile nyumba, magari na biashara kwa ajili ya kuwalinda na majanga mbalimbali kama moto na n.k

"Tembelea banda letu hapa ujipatie huduma ya bima ili uweze kujilinda wewe na Rasilimali zako . Aidha tumeboresha mikopo ya wafanyakazi wa taasisi za umma na binafsi na baadhi ya maboresho ni Pamoja na muda wa marejesho ambao ni mpaka miaka 7 ,viwango vya mikopo , muda mfupi wa kupata mikopo na mikopo ya muda mfupi (Salary advance) N.k

Banda la Benki ya Akiba linapatikana Sabasaba Hall katika Viwanja vya maonesho ya kimataifa sabasaba .





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...