Na Janeth Raphael
Waziri wa kilimo Hussein Bashe amezindua kituo cha huduma kwa wateja wakulima, kitakachowawesha wakulima kupiga simu bure kupata taarifa za kilimo,ikiwemo kutatuliwa changamoto zao na wataalamu wa sekta hiyo.

Bashe alisema hayo leo,wakati wa uzinduzi wa kituo hicho uliofanyika  jijini Dodoma huku baadhi ya wakulima wakishuhudia uzinduzi huo.
Bashe alisema,wakulima watakuwa wakipiga simu  bure ili kupata taarifa na kuuliza maswali yanayohusiana na kilimo lengo likiwa ni kuwafikia wakulima popote walipo nchini.

Amesema jambo hilo ni mwanzo wa kuelekea hatua kubwa ya mafanikio ambapo wakulima watakuwa wakipata  taarifa ya mazao gani yanatakiwa sokoni ili waweze kulima kwa wingi.
"Wakulima watakuwa wakipiga simu bure namba ya huduma kwa wateja ambayo ni 0733800200  itakayomfikisha moja kwa moja kwa watendaji,"alisema Bashe.

Waziri Bashe Amefafanua zaidi ya kuwa, awali walikuwa wakisikiliza matatizo ya wakulima kwa njia ya ujumbe mfupi,lakini sasa yatasikilizwa kwenye simu ikiwemo kuwa na mfumo unaotunza taarifa za wateja ambazo kama swali halijajibiwa muda huo litapata fursa ya kuijbiwa.

Bashe alisema kuwa baada ya mfumo wa huduma kwa wateja kukamilika kama nchi lazima kuwe na kitengo kilichosajiliwa cha masoko ili kuangalia bei kwenye soko zinakwendaje .

Alisema ifike mahali wizara iwe na kitengo chenye nguvu cha kuingia kutafuta masoko ili kufanya mazao yetu ya we na ushindani kwenye soko.
Hata hivyo waziri Bashe aliahimiza Kituo hicho kufanya kazi masaa 24 na kuwe na mfumo unaotunza taatifa.

Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde alisema kuwa Kazi kubwa imefanyika katika kuiweka Wizara ya Kilimo kiganjani.

Amesema kuwa mkakati uliopo ni kuanzishwa kwa channel maalum kwa ajili ya Kilimo.
Alisema kuwa kupitia Kituo cha huduma kwa wateja wakulima watapata taarifa za kilimo kila siku na wakulima wengi watafikiwa.

Katibu wa wizara hiyo Andrew Masawe alisema takwimu zinaonyesha mfumo wa M Kilimo umesaidia kaa kiasi kikubwa wakulima,huku wakifanikiwa kusajili wakulima milion 5.5 kupitia mfumo huo,wakati wauzaji wa nje waliosajiliwa ni 3905.
Masawe alisema tayari wametatua changamoto 60,120 za wakulima.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo, Katibu Mkuu wa wiz Wizara ya Kilimo wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji kazi wa kituo cha huduma Kwa wateja kilichozinduliwa Leo jijini Dodoma.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akizungumza na mmoja wa wakulima mara Baada ya uzinduzi wa kituo cha huduma Kwa wateja
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akisisitiza jambo kwa watengaji kazi walipo chini ya ofisi yake
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha huduma Kwa wateja


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...