Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mpanda, Jeff Shantiwa akimuonesha Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete maeneo mbalimbali ya Kiwanja cha Ndege Cha Mpanda wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea kiwanja hicho mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mpanda Jeff Shantiwa (katikati) na Meneja wa Kampuni ya Ndege Nchini (ATCL) Peter Kilawe mara baada ya kutembelea Kiwanja cha Ndege Cha Mpanda mkoani Katavi.

Muonekano wa Barabara ya Kuruka na Kutua Ndege ya Kiwanja cha Ndege cha Mpanda Mkoani Katavi.


NAIBU Waziri wa Uchukuzi Atupele Mwakibete ameitaka Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kutazama upya gharama za tiketi kwa safari za ndani ya nchi ili kuvutia wasafiri wengi kutumia usafiri wa shirika hilo.

Akizungumza mkoani Katavi baada ya kutembele Kiwanja cha Ndege cha Mpanda Naibu Waziri Mwakibete amesemaa uwepo wa gharama kubwa za tiketi unachangia uchache wa abiria wanaotumia shirika hilo pamoja na takwimu kuonyesha ongezeko la abiria kwa safari za ndani kupitia kiwanja hicho.

“Takwimu nilizosomewa hapa zinaonyesha ongezeko la abiria kwa safari za ndege lakini naambiwa hapa abiria bado wapo wa kutosha lakini wanakwazwa na na gharama za nauli, mkiangalia upya nina Imani mnaweza kuleta ndege karibu kila siku ‘ amesema Naibu Waziri Mwakibete.

Naibu Waziri Mwakibete amesema Serikali imeichukua changamoto ya udogo wa jengo la abiria kiwanjani hapo na kuahidi kuwa itatafuta fedha ili kujenga jengo litakaloendana na hadhi ya kiwanja hicho.

Aidha, Naibu Waziri Mwakibete amewataka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) kujenga barabara itakayotumika kukagua eneo lote la kiwanja ili kupunguza changamoto za shughuli za kibinadamu zinazohatarisha usalama kiwanjani hapo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusufu ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuhakikisha ATCL inaongeza safari zake mkoani humo kutoka safari moja kwa wiki mpaka kufikia safari nne kwa wiki uamuzi uliorahisisha shughuli za kibiashara biana ya mkoa huo na mikoa mingine.

Kwa upande wake Meneja wa Kiwanja cha Ndege Mpanda Jeff amesema TAA inaendelea kuhakikisha kiwanja hicho kinatoa huduma stahiki kulingana na kanuni na taratibu za usafiri wa Anga Duniani.

Meneja wa ATCL Mkoa wa Mpanda Salehe amesema pamoja na changamoto za kiwanja kutokuwa na kituo cha mafuta ATCL itaendelea kutoa huduma huduma bora na za viwango kupitia kiwanja hicho.
(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uhchukuzi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...