Na Mwandishi Wetu,Njombe

MAKAMU wa Rais wa Shirika la Dawa Asili Tanzania Tameto, Islam Makingili ambaye pia ni Mtafiti wa dawa za asili amewataka Watanzania kukitumia kituo cha Islam Herbal Medicin Center kilichopo Makambako mkoani Njombe ili kutibu maradhi yanayowasumbua yakiwemo ya kuvunjika mifupa.

Makingili ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Waganga wa Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA) ameeleza kupitia dawa za tiba asili waliovunjika mifupa wanapona na kurejea katika hali ya kawaida na kuendelea na shughuli za kawaida.

Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisini za kituo hicho zilizopo katika mji wa Halmashuri ya Makambako Mtaa wa Posta, ambapo amesema watanzania wengi wanakabiliwa na maradhi mbalimbali kwenye miili yao hivyo kupitia kituo hicho wanatibu maradhi hayo.

Amesema kituo cha Islam Herbal Medicin Center inaunga mifupa kwa wale wanaovunjika pia wanatibu magonjwa sugu yaliyoshindikana hata katika hospitali za kawaida kama vile kaswende,Gono,Uti,vidonda vya tumbo na hata kansa.

Amewataka wagonjwa hao kwenda na vipimo ambavyo wamepima katika hospitali kwa lengo la kujiridhisha kabla ya kuwapatia huduma."Kwa kifupi nimeaza shughuli hizi tangu miaka ya 1973 nikiwa kijana mdogo hadi sasa hivyo nina uhakika na kile ambacho ninakifanya.

"Na katika kipindi hicho chote sijawahi kukutana na changamoto zozote zaidi ya kuokoa maisha ya watu kutokana na maradhi wanayokabiliana nayo."amesema Makingili

Ameongeza pamoja na  mengine pia ni mtafiti na kwamba ili uwe mganga mzuri lazima ufanye tafiti za kutosha,  hivyo katika hilo amejiridhisha kwa asilimia 100 kuhusu  dawa ambazo anawatibia watu na kwa bahati nzuri wagonjwa wenyewe wanaleta shuhuda baada ya kupona.

Akizungumzia zaidi kuhusu huduma hiyo Makingili amesema licha ya uwepo na kituo hicho mkoani Njombe lakini pia anakituo kama kingine mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea mjini ambapo pia wanaunga mifupa na kutoa huduma zingine kutokana na maradhi mbalimbali yanayowasumbua binadamu.

Aidha amesema licha ya kutibu Kasendwe,Gono,Vidonda vya Tumbo, Kansa pia anatibu kizazi kwa wanawake anazibua mishipa na kuimarisha mishipa hiyo kwa upande wa wanaume na hiyo ni kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo msongo wa mawazo (stress) kipato, nakadhalika.

" Naomba nitumie nafasi hiyo kutoa Rai kwa Watanzania wenye kusumbuliwa na maradhi mbalimbali wafike kwenye kituo chetu na wale ambao wanahitaji ufafanuzi wa masuala mbalimbali wanaweza kuwasiliana nasi kupitia namba za simu 0768337248 au 0715542028," amesema Tabibu Makingili.

Ameongeza kwamba ",Nataka nieleze kuwa mafanikio  yote ambayo yapatikana yanatokana na kufanya kazi kwa kufuata utaratibu na sheria zinazotuongoza kwa mfano mimi hapa nina usajili na ninafanya kazi zangu kwa kufuata misingi ya vibari niliovyonavyo.

Amesisitiza kwamba kama kuna mgonjwa ambaye hali yake hairidhishi basi awanawasiliana na ofisi ya mganga mkuu na wanakwenda kumchukua na kisha  kumpatia huduma zingine na kimatibabu na hata wale wanaoshindikana hospitalini wafike kwake.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...