Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

BONDIA Wa Ngumi Za Kulipwa Nchini anaewakilisha Arusha  Shaban Ndalo a.k.a CMG atupa kete yake dhidi ya mpinzani wake Selemani Galile  kuelekea katika Pambano La "Ubabe Ubabe Tu" Septemba 24 mwaka huu Mkoani Mtwara

Ndalo amesema anaendelea na Maandalizi vizuri Kwa Sasa Huku akimkimgia kifua na kumpa tambo kuwa Seleman Galile kipigo atakachokutana nacho kitadhihirisha kuwa Arusha kuna mabondia wazuri zaidi ya mikoa mingine.

Kwa Upande wa kocha wa bondia huyo Makelena Nyimitika kutoka "under tower Gym" amesema Wakazi wa Arusha pamoja na wa Tanzania wategemee Burudani ya aina yake huku akiahidi Ushindi wa mapema wa "Ko".

Hata hivyo Nyimitika amesema Bondia wake alikua na kiu ya kutaka kupanda ulingoni Kwa muda mrefu na Bondia yoyote yule ila kiu yake kubwa ilikua ikimuhitaji sana Dulla mbabe hivyo ametoa ahadi kuwa wakimalizana na kipigo Kwa Galile Mashabiki zake watarajie kupanda ulingoni na Dulla mbabe.

Bondia huyo atapanda ulingoni usiku huo kupepetuana dhidi ya Seleman Galile katika Pambano la raundi sita huku Pambano kuu likiwa la Mwamba kutoka Morogoro Mzee wa "Show show" Twaha kiduku akionesha Ubabe Ubabe Tu Septemba 24 mwaka huu Mkoani Mtwara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...