Katibu Mkuu wa Utamaduni Sanaa na Michezo dkt.Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wahabari na wadau wa Sanaa nchini kuelekea Tamasha la Sensabika linalotarajiwa kufanyika agosti 21 katika viwanja vya leaders club jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha Kampeni ya uhamasishaji wa zoezi la sensa ambapo Tamasha hilo litahudhuriwa na wasanii kutoka Mashirikisho mbalimbali.
Sehemu ya Marais kutoka katika Mashirikisho mbalimbali akiwemo Cynthia Henjewele kutoka Shirikisho la ushereheshaji na mapambano ,kushoto kwake akiwemo Ado Novemba kutoka Shirikisho la Muziki nchini wakisikiliza kwa makini taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Utamaduni Sanaa na Michezo dkt.hassan Abbasi mara baada ya kutangaza Tamasha la Sensabika linalotarajiwa kufanyika agosti 21 katika viwanja vya leaders club jijini Dar es salaam kabla ya kufikia siku ya Sensa agosti 23 Huku akisisitiza wananchi kutulia katika kaya zao kusubiri kuhesabiwa
 
    

Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

TAMASHA la  Sensabika kuhitimisha Kampeni ya uhamasishaji wa zoezi la sensa huku likikutanisha Sanaa mbalimbali nchini kuonyesha uzalendo na pamoja na jamhuri ya watu wapambanaji kwenye Taifa lao.

Akizungumza na waandishi wahabari pamoja na wadau wa Sanaa jijini Dar es salaam,Katibu Mkuu wa Utamaduni Sanaa na Michezo  dkt.Hassan Abbasi amesema awali kulikua na zoezi la uhamasishaji Kwa njia ya Kidigitali ambapo watu katika Sekta mbalimbali wameweza kushiriki kikamilifu kwa kuchapisha picha zenye ujumbe wa kuhamasisha sensa na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika uhamasishaji huo wa Kidigitali hivyo ni zamu ya Sekta ya Sanaa kutoa burudani mbalimbali jukwaani katika kutamatisha zoezi hilo la uhamasishaji.

"Tumeona jambo letu lisiishe kimya kimya tutumie Sanaa zetu kuhakikisha jamhuri ya wazalendo tunasherehekea kiburudani zaidi kutoka katika Mashirikisho mbalimbali ikiwemo shirikisho la Sanaa za ushereheshaji na mapambano, shirikisho la Sanaa la uchoraji, Ubunifu, shirikisho la Sanaa la Muziki pamoja na shirikisho la Filamu nchini kutumia jukwaa la "Sensabika" kutoa burudani siku ya agosti 21 siku 1 kabla ya siku yenyewe rasmi ya kuhesabiwa katika kaya zetu."

Hata hivyo amesema kuwa ni vyema watu kutulia katika makazi yao  kusubiri zoezi hilo la kuhesabiwa Huku akiongeza kuwa wasanii wameongezewa siku 3 kuwasilisha kazi zao za kisanaa ili kupewa nafasi katika Tamasha hilo kutumbuiza ambapo awali dirisha la kupokea kazi hizo lilifungwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Pia akatoa rai kuwa zoezi la uhamasishaji wa kitu chochote chenye Maendeleo wataendelea kuwatumia Wasanii kwani wana nguvu shawishi sana katika jamii.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Philemon Mapana amesema kuwepo Kwa Tamasha hilo kuanenda kuwapa fursa wasanii wote pamoja na wana michezo kushiriki kikamilifu katika kuandika historia ya kizalendo katika taifa la Tanzania.

Huku akitilia mkazo kuwa Baraza litapokea kazi za sanaa ambazo zenye umahili zaidi hivyo wasanii wafanye vitu vyenye Ubunifu zaidi kutokana na Tamasha hilo litakuwa linaonekana kitaifa na Kimataifa.

Hata hivyo Rais wa shirikisho la Sanaa na ushereheshaji na mapambano Cynthia Henjewele amepongeza wizara kwa kuona umuhimu wa Mashirikisho ya Sanaa zote kushiriki katika uhamasishaji wa zoezi la sensa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...