Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limefadhaishwa na kauli iliyotolewa na Mmiliki wa timu ya Napoli FC ya Italia, Aurelio De Laurentiis akidai kuwa timu yake haitosajili Wachezaji kutoka barani Afrika, kwa kuwa Wachezaji hao wanachangia timu yake kufanya vibaya wakienda kwenye timu zao taifa.

Hivi karibuni, Mmiliki huyo alinukuliwa na mitandao mbalimbali ulimwenguni akitoa kauli hiyo kufuatia kuwakosa kwenye timu yake, Wachezaji, Kalidou Koulibaly (sasa Chelsea) kutoka Senegal na Kiungo wa Cameroon, Andre Zambo Anguissa, kufuatia Wachezaji hao kuwa kwenye majukumu ya timu za taifa kwenye Michuano ya AFCON nchini Cameroon mapema mwaka 2022.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CAF mapema Agosti 7, 2022, imeeleza kuwa kauli hiyo haikubaliki na imekiuka Kanuni za Maadili ya Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) huku wakilitaka Shirikisho hilo kufanya uchunguzi juu ya kauli hiyo.

CAF imeeleza kuwa mchezo wa mpira wa miguu unachezwa barani Afrika, Ulaya, Kaskazini na Kusini mwa Amerika, na hata bara la Asia, huku ikibainisha kuwa mchezo huo unawaleta watu mbalimbali pamoja kupitia tamaduni zao, lugha, dini na masuala mbalimbali ya muingiliano wa kijamii.

Hata hivyo, CAF wamehoji juu ya kauli hiyo ya De Laurentiis: “Je zuio hilo litagusa pia Wachezaji wengine wanaotoka kwenye Mabara ya Amerika Kusini, Asia na Mabara mengine kucheza mashindano yao? Je kama ni hivyo, hayo yatakuwa maendeleo ya soka na kukua kwa soka ulimwenguni?”.

Mwisho, CAF wamemalizia kusema kuwa Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) ni alama ya bara la Afrika na mashindano mengine ulimwenguni, mara ya mwisho kufanyika kwa AFCON nchini Cameroon, zaidi ya Mataifa 160 yalishuhudia na kuvutia zaidi ya Watazamaji Milioni 600 ulimwenguni kote.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...