Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
WIZARA
ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Wizara ya Fedha na
Mipango zimeziagiza kukaa kwa pamoja kujadiliana namna ya kuhakikisha
ujenzi wa Stendi katika Manispaa ya Moshi unakamilika kwa haraka kwani
wananchi wamesubiria kwa muda mrefu bila mafanikio.
Ushauri huo
umetolewa leo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo
alipokuwa akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Moshi mkoani
Kilimanjaro ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa ujenzi wa stendi
hiyo ulianza mwaka 2018 na ulitakiwa kukamilika mwaka 2020 .
“Na
mpaka leo stendi haijakamilika , bado wasafiri wanajibana kwenye stendi
ya zamani na sababu za msingi hakuna huyu anasema ilikuwa hivi , mara
kimeenda vile , kimerudi pale, lakini sababu zinazotolewa hazisaidii
kutatua changamoto za wananchi.Naagiza Wizara zinazohusika na hili jambo
TAMISEMI na Wizara ya Fedha wakae wakubaliane namna kumaliza stendi kwa
haraka.
“Wananchi hawataki maneno hatawaki hadithi, wanachotaka
ni huduma iliyokusudiwa itolewe kwa wakati , tuliwahiwaadi kuwajengea
stendi na stendi imeenza na fedha zimetolewa kwa kiwango fulani ,
nipongeze Serikali kwa kutoa fedha kiasi fulani.
“Nimeambiwa
tayari Sh.bilioni saba mpaka tisa na zimeshatolewa na sasa zinahitajika
zifike Sh.bilioni 17 ili stendi iweze kukamilika , mwanzo katika ujenzi
ilitakiwa kujengwa na jengo la hoteli hivyo ikawa inatakiwa Sh.bilioni
28, sasa wametoa hoteli zinatakiwa Sh. bilioni 17 ili stendi ianze kutoa
hduma za kisasa.
“Wananchi wanaosafiri na hasa kwenye Manispaa
hii ya Moshi lazima hiyo stendi tuifikishe huko , iondoke ilivyo sasa
iwe uhalisia, nataka niwahakikishie jambo hili nitalibeba na
nitalifikisha kwa wahusika na leo nimezungumza na Waziri wa TAMISEMI
amenihakikishia jambo analishughulikia wanaendelea na mawasiliano na
Hazina ili fedha zishuke huku.
“Na agizo langu litawafikia hata
kabla sijafika, sisi ndio wenye Ilani hatutaki ifike mwaka 2025 kuja
kuulizwa tena stendi , tunataka stendi ya Moshi ikamilike watu waanze
kuitumia ili tuanze mipango mingine na sio hadithi za muda mrefu za
stendi,”amesema Chongolo.
Ameongeza kuwa yeye amepewa dhamana ya
kumsaidia Mwenyekiti ambaye ndio Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
, hivyo hawezi kukubali kuja kukutana na maswali ambayo majibu yake ni
rahisi kwani yanataka utekelezaji.
“Niwahakikishie tutavutana
mashati , tutavutana huko waliko ili waje watekeleze lifike mwisho,
hatutaki kuwa na miradi ambayo inakaa kwenye makaratasi muda mrefu. Ni
lazima tuifikishe ukomo ili tuhangaike na mambo mengine, na hili na
libeba mimi, kesho mniulize mimi na nitaendelea kulisukuma nikiona
linanishinda nitakwenda kumwambia Mwenyekiti wetu watu wako
wananishinda, na ninyi mnavyonona hivi naona ni mtu wa kushindwa?”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...