
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MKUU
wa Wilaya ya Kibaha,Sara Msafiri ameeleza wanatarajia kufanya matamasha
na kutoa elimu ya umuhimu wa Zoezi la sensa kupitia nyumba za ibada ili
kuongeza wigo wa elimu ya sensa ndani ya jamii.
Vilevile,
ameiasa jamii yenye watoto wenye ulemavu mbalimbali kuwatoa watoto wao
kushiriki kuhesabiwa siku ya sensa pasipo kuwaficha ili kupata idadi
kamili ya watu wenye makundi maalum ,baadae wapate kujulikana idadi Yao
kamili na kupangiwa mipango ya kimaendeleo Kama ilivyo kwa wasio na
ulemavu.
Sara
Msafiri alibainisha Mjini Kibaha ,kwamba watatumia pia viongozi wa
dini na maeneo ya ibada ili japo dakika mbili zitumike kuwapa Uelewa na
kujua umuhimu wa Zoezi hilo kwa waumini.
Aidha
alisema mgawanyo wa rasilimali hauko sawa kutokana na kutokuwa na
takwimu sahihi ya watu,hivyo Zoezi hilo likifanikiwa kwa asilimia 100
litaleta tija kiwilaya,mkoa na Kitaifa .
Pamoja
na hayo ,akiwa Mlandizi Sara alizungumza na viongozi wa madereva
pikipiki (bodaboda, )viongozi wa soko na wausafirishaji wa daladala
katika kikao chake cha kujadili namna ya kuhamasisha kushiriki sensa.
Alisema
ili mgawanyo uende sawa na kila mmoja apate huduma stahiki ni vema
wananchi washiriki kuhesabiwa ifikapo Agost 23 Serikali iweze kupeleka
huduma inayoendana na idadi ya watu.
"Wilaya
ya Kibaha ilikuwepo katika sensa ya majaribio ,itakuwa haipendezi
tukashindwa kusimamia kikamilifu Zoezi la sensa linalokuja "alieleza.
"Rais
amewekeza kwenye anuani za makazi na sensa ya watu wananchi tutoe
ushirikiano kwa maharani wa sensa, nimewaita nyie ili mnisaidie
kuhamasisha na wataalamu wataendelea kutoa elimu kila mahali kuhusiana
na umuhimu wa hili jambo" Alifafanua Sara.
Hata
hivyo ,Sara aliwataka wafugaji kuondokana na dhana ya kwamba mifugo
ikihesabiwa inakufa badala yake waruhusu kuhesabiwa wao na mifugo yao
ili dawa za mifugo ziweze kutolewa za kutosheleza idadi iliyopo.
Mkuu
huyo wa Wilaya ,alimuelekeza Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya
Kibaha kuitisha kikao na wanawake ili waweze kupatiwa elimu ya sensa
kwani wao ni watu wenye ushawishi kwenye jamii.
Kwa
upande wake ,Mkufunzi wa sensa wa Halmashauri hiyo Gele Msangi
aliwataka wananchi kuzingatia kutoa taarifa sahihi kwa maharani wa
sensa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...