Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM,) Daniel Chongolo akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya na nyumba ya watumishi katika Kata ya Masama Rundugai Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro.

 Katibu Mkuu wa Chama cha Mainduzi (CCM,) Daniel Chongolo akisikiliza taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kutoka kwa Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Dkt. Itikija Msuya mara baada ta kukagua mradi huo.

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM,) Daniel Chongolo amekagua utekelezaji wa  Mradi wa kituo cha Afya na nyumba za watumishi katika Kijiji cha Chemikaji Kata ya Masama Rundugai wilayani Hai huku ikielezwa kuwa, mradi huo utatatua changamoto ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya pamoja na kuwasaidia akina Mama wajawazito wanaohitaji huduma za upasuaji na kupunguza vifo vya akina Mama wajawazito na watoto wachanga.

Mradi wa ujenzi wa kituo hicho ulianza kujengwa kwa nguvu za Wananchi kwa kuchangia shilingi Milioni 11 na Halmashauri kuchangia  shilingi milioni 28.

Aidha mbali ya fedha hizo, Serikali awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan imetoa Kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho hadi sasa nyumba za watumishi zimekamilika kupitia fedha za UVIKO-19 zipatazo milioni 90 zilizotolewa na Serikali Desemba mwaka jana. 

Ujenzi wa Kituo hicho unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba 30, 2022.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akikagua majengo ya kituo cha afya ya Kata ya Masama, Hai Mkoani Kilimanjaro.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipanda mti katika kituo cha Afya Masama Rundugai wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.




Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akikabidhiwa fimbo ya kimasai baada ya kuvalishwa vazi la kimila alipofika kukagua mradi huo wa kituo cha Afya ambao utasaidia upatikanaji wa huduma za Afya kijijini hapo.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na baadhi ya akina Mama baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya na Nyumba za Watumishi katika kata ya Masama Rundugai kijiji cha Chekimaji wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro.
Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe.Sashisha Mafue akizungumza jambo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM ,Daniel Chongolo mara baada ya kukagua majengo ya kituo cha afya ya Kata ya Masama, Hai Mkoani Kilimanjaro.
Katibu MKuu wa CCM Daniel Chongolo na Ujumbe wake wakifurahia jambo
Wakaazi wa eneo la Masama wakifurahi jambo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...