Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Titus Kaguo akimsikiliza mwananchi aliyetembelea banda la EWURA katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane 2022 yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV , Mbeya
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa upo utaratibu wa kuomba leseni ya rejareja ya biashara ya mafuta lengo ikiwa kulinda usalama wa mafuta kwa watumiaji.
Hayo aliyasema Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa AWURA Titus Kaguo wakati akizungumza na Michuzi Blog kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Amesema kuwa EWURA inaangalia usalama wa mafuta kwa watumiaji hivyo kufanya biashara ya mafuta bila leseni ni kosa la kisheria kutokana na kanuni za uendeshaji wa biashara ya mafuta ya rejareja za mwaka 2022 zinamtaka mafanyabiashara ya mafuta ya petroli wa rejareja aombe leseni kutoka katika mamlaka hiyo.
Kaguo amesema taarifa muhimu zinazohitajika kuomba leseni ni nakala ya nyaraka za usajili wa kampuni au leseni ya biashara, Hati ya Miliki ya Kiwanja palipojengwa kituo cha mafuta au udhibitisho mamlaka husika iliyoruhusu ujenzi wa kituo hicho , Kibali cha ujenzi kutoka Halmashauri au Manispaa husika , Cheti cha tathimini ha athari ya mazingira , Nakala ya Cheti cha Mlipa kodi, Nakala ya cheti cha zimamoto.
Amesema utaratibu mwingine kibali cha ujenzi kutoka EWURA kwa vituo vilivyojengwa baada ya Aprili 2009, Orodha ya miundombinu iliyopo katika eneo , Mchoro wa Kituo ambao umesainiwa na mhandisi aliyesajiliwa na Baraza la Wahandisi Tanzania, Stakabadhi ya malipo ya ada na maombi ya kibali cha ujenzi ambayo ni 500, 000.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...