Wakati Maonyesho ya nane nane yakiendelea katika viwanja vya Jonh Mwakangale jijini Mbeya kampuni ya uuzaji wa magari na mitambo ya GF Trucks & Equipments Ltd imezindua kauli mbiu ya Kilimo Usarishaji katika viwanja hivyo yenye lengo la kuhamasisha wakulima kupata usafiri bora wa mazao yao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja masoko na mawasiliano wa kampuni hiyo Smart Deus alisema kampuni hiyo imekuja na mkakati wa kuwakomboa wakulima wadogo na wajasiliamali kwa kuzindua gari mpya tani 4 aina ya FAW CA1073 maalumu kwa ajili ya kubebea mizigo midogo ambayo itawasaidia wakulima kutolea mizigo mashambani na kuipeleka katika magulio na masoko

Pia GF wanazo gari maalumu kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji hali ambayo itamwezesha mkulima kuendelea na shughuli za umwagiiliaji hata kama eneo husika maji ya uhakika na hasa kipindi cha ukame Unajua kwa sasa Magari ya FAW yanatengenezwa nchini Tanzania katika kiwanda chetu kilichopo Kibaha mkoni Pwani hivyo kwa kununua magari haya itawezesha serikali kuokoa pesa za kigeni zilizokua zikitumika kuagiza magari kutoka nje ya nchi hali inayosababisha bei yetu kuwa rafiki tofauti na hapo awali alimaliza Smart Deus Meneja Masoko.

Kwa upande wa mmoja wa wakulima wa vitunguu katika bonde la Ruaha Iringa ,Samsoni Mwakibete alisema ujio na uzinduzi wa gari hiyo utawarahisishia wakulima katika shunghuli zao

Gf wanampango maalumu wa kuwakopesha vitendea kazi wakulima kwa kushirikiana na Benki rafiki ambapo mkulima akikidhi vigezo atapatiwa mkopo wa huo na Benki itamlipia na dhamamana itakuwa kifaa hicho ambapo yeye na benki watamalizana wakati tayari anaendelea kufanyia kazi.


Meneja Masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s ltd, Smart Deus akiwakabidhi zawadi ya fulana washindi wa shindano la Kilimo Usafirishaji lililofanyika katika viwanja vya nane nane jijini Mbeya wakati wa uzinduzi wa gari maalumu kwa wakulima lenye kauli mbiu ya Kilimo na Usafirishaji
Afisa mauzo wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s ltd, Poul Msuku akigawa zawadi ya Tishet kwa mmoja ya mteja aliyefika bandani kwao wakati wa uzinduzi wa gari maalumu ya wakulima yenye kauli mbiu ya KILIMO USAFIRISHAJI katika viwanja vya nane nane jijini MbeyaMichuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...