Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Dk.Cairo Mwaitembe akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Chuo hicho kwenye maonesho ya kilimo kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Mwananchi akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Chuo cha Uhasibu Arusha kwenye Maonesho yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

*Yabainisha kozi ya uhasibu kwa wakulima ndio suluhisho kwao

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mbeya
MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA) Dk.Cairo Mwaitembe amesema chuo cha uhasibu ni chuo pekee kinachoweza kufanya wakulima wakuwe kiuchumi.

Dk.Mwaitembe ameyasema hayo kwenye banda la chuo hicho katika maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea viwanja John Mwakangale Jijini Mbeya amesema wakulima wakisoma watajua kupanga hesabu zao pamoja na kuongeza thamanj ya mazao.

Amesema Chuo Uhasibu Arusha (IAA) kina kozi kwa ambayo wakulima ni wakati wa kwenda katika kilimo biashara na kujua hesabu na kupanga namna ya soko linavyokwenda.

Dk.Mwaitembe amesema kuwa kozi ya shahada ya pili wanafundisha mwaka mmoja ambapo ndio chuo pekee kinachotoa hivyo ni fursa kwa watanzania kuongeza utaalam.

Amesema kozi hiyo walichukua uzoefu nchini Uingereza na kufanikwa kuendesha kwa muda mfupi hata kwa walio kazini wanaweza kusoma kutokana na kufundisha kwa njia ya mtandao.

Aidha amesema kuwa wanafunzi wanye mawazo ya ubunifu wana atamizi ya kulea ubunifu na kuendeleza mawazo hayo.

Hata hivyo amesema Chuo kimekuwa kikitoa elimu bora yenye kukidhi soko la ajira katika fani mbalimbali zilizopo chuoni hapo na kuongeza Nane Nane ni sehemu muhimu kwa wakulima na wafugaji kutembelea na kuweza kujiunga katika kozi ya uhasibu ya kwenda kuleta mapinduzi ya kilimo biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...