Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV-Tanga

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo akiwa na viongozi wengine wa Chama na Serikali amekagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya Bandari ya Tanga yenye lengo la kuiwezesha bandari hiyo kuwa na uwezo mkubwa wa kupokea na kusafirisha mizigo mikubwa kupitia kwenye meli kubwa katika ukanda wa Bahari Kuu.

Akizungumza leo Agosti 12,2022 , Katibu Mkuu wa CCM Chongolo amesema mradi huo unakwenda kubadilisha matokeo ya usafiri na usafirishaji kwa kutumia maji kwenye ukanda huo ambapo wao ambao wamepewa dhamana ya kuratibu kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA).

“Uwezo wa awali wa bandari hii  ni tani kama 700,000 lakini sasa baada ya kukamilika hii yote zitakuwa zinaingia meli mbili kwa wakati mmoja ambazo zitakuwa  zinatia nanga hapa na uwezo wa bandari utakuwa tani milioni tatu.Hayo ni maendeleo makubwa , tani milioni tatu zikishuka maana yake itakuwa ni mara tatu au mara nne ya tani za awali,”amesema Chongolo.

Amefafanua kwa hiyo maana yake wanategemea kuona mageuzi na maendeleo ya kasi ya mara tatu na nusu au na zaidi yaliyopo sasa lakini kilichomfurahisha zaidi ni kutengenezwa kwa kina cha maji kutoka mita tatu kwenda mita 13.

 “Kikubwa sasa huduma itakayotolewa ifanane na hayo maboresho yanayofanyika, wote mnajua hii bandari ni bandari kubwa , ni bandari ya historia, ndio bandari iliyopo katikakati ya bandari kuu ya Dar es Salaam na Bandari Kuu ya Mombasa, kwa hiyo hii ndio bandari ya historia ya Afrika Mashariki ambayo tunaweza kujivunia.

“Kwani imejitengeneza kimkakati kwenye biashara, ni bandari ambayo inajitafsri inaweza kuleta biashara kati yetu na maeneo mengine ya ndani ambayo yamejifunga hanaya ukaribu na bandari.

Kwa upande wake  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga amewatia moyo na shime wanaohusika na utekelezaji wa mradi huo wa ujenzi wa miundombinu ya kuongeza uwezo wa kutoa huduma na matumaini makubwa ya Watanzania ni vyanzo vyote vya mapato vya kujenga maisha yao.

“Watanzania wanataka maisha mazuri na hayaji kwa nadharia bali kwa kitu gani unazalisha, kwa hiyo ni mpongeze Meneja wa Bandari ya Tanga kwa usimamizi wa ujenzi huu na tumeoneshwa sehemu zote ambazo zinatuletea neema, hivyo kikubwa tuendelee kuwaombea ili waendelee kuwa na moyo wa kizalendo,”amesema Kanali Lubinga.

Wakati huo huo Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Athuman Mrisho amesema matarajio yao yao Novemba 28 mwaka huu mradi huo utakabidhiwa wote ambapo jumla ya gati zao mbili zitakuwa na urefu wa mita 450 , hivyo watakuwa na uwezo wa kuingiza meli mbili kubwa zenye urefu wa kila mmoja mita 220.

Kuhusu faida itakayopatikana baaada ya kukamilika kwa marekebisho hayo kwanza itakuwa urahisi wa kushusha na kupakia mizigo kwani kwa sasa inabidi wapakue mzigo mara mbili kutokana na meli inaposimamia na mzigo unapotakiwa kufika.

“Meli ya mizigo ilikuwa inakuja na kupakua  mizigo kwenye tishali halafu inavutwa inakuja hapa , kwa hiyo kuna kitu kulikuwa kinafanyika, kwa maana kupakuliwa mara mbili ni gharama hiyo kwa hiyo sasa  tutaweza kuhudumia meli kubwa moja kwa moja.

“Faida ya pili itakuwa ni kupunguza gharama, ilikuwa lazima ulipie ile gharama ya kupakua mara mbili, kwa maana tukupinguza hizo gharama tutaongeza wateja.

"Sisi kwa mwaka bandari yetu ya Tanga tunahudumia tani 7.8 lakini kukamilika kwa mradi huu tutaweza kuhudumia hadi tani milioni tatu,”amesema Meneja huyo wa Bandari ya Tanga.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Bandari Tanga Ndugu  Masoud Athuman Mrisho (kushoto) mara baada ya kutembelea bandari ya Tanga na kujionea maboresho yatakayosaidia kupokea meli kubwa za mizigo.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Bandari Tanga Ndugu  Masoud Athuman Mrisho (kulia) mara baada ya kutembelea bandari ya Tanga na kujionea maboresho yatakayosaidia kupokea meli kubwa za mizigo.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiongozana na Meneja wa Bandari Tanga Ndugu  Masoud Athuman Mrisho pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Chama wakati wa kukagua maendeleo ya upanuzi wa bandari ya Tanga utakaowezesha meli kubwa za mizigo kutia nanga.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Bandari Tanga Ndugu  Masoud Athuman Mrisho (kushoto) mara baada ya kutembelea bandari ya Tanga na kujionea maboresho yatakayosaidia kupokea meli kubwa za mizigo.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...