Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema dhamira ya dhati ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuitazama kwa karibu sekta ya kilimo, ikiwemo kuongeza bajeti ya Wizara Kilimo, kutoka sh. Bilioni 254 mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sh bilioni 954 sawa na asilimia 224 kwa 2022/2023, italeta mabadiliko makubwa katika uchumi.

Miongoni mwa mabadiliko hayo ni pamoja na kutengeneza fursa nyingi za ajira ambapo kufikia 2025 vijana na wanawake zaidi ya milioni 3 watanufaika na ajira hizo, hatua ambayo imemfanya Shaka atoe m
uelekeo wa kutatua changamoto ya ajira kwa vijana hususan wasomi wa vyuo vikuu ambao ametaka watambuliwe na kuwezeshwa kupitia kilimo.

Shaka amesema hayo leo Agosti 7, 2022 alipotembelea Maonesho ya Kilimo (Nanenane) Kanda ya Mashariki yanayofanyika mkoani Morogoro ambapo amesema kupitia maonesho hayo lipo jambo la faraja ambalo ameliona.

“kuonesha mkazo zaidi katika Serikali hii ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza nguvu kwenye sekta ya Kilimo na dhamira kubwa ikiwa kuwakomboa vijana pamoja na wanawake”.

Aidha amesema kuwa maelekezo ya Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2020 - 2025 katika Ibara ya 8 kifungu f imeahidi katika kipindi cha miaka mitano kutazalishwa ajira milioni nane kwa Watanzania, sasa kwenye kutafsiri maelekezo ya Ilani Serikali ya Rais Samia imeshajiwekea mwelekeo ama imeshajiwekea matatarajio yake katika ajira hizo kupitia sekta ya kilimo.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...