MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wamefika salasala Jijini Dar es salaam nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema ili kutoa pole na kuifariji familia, ndugu , jamaa na marafiki kufuatia kifo cha kiongozi huyo aliyefariki 21 Agosti 2022 katika hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.

Akiwa nyumbani hapo, Makamu wa Rais amewapa pole wana familia na kuwaomba kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu. Makamu wa Rais amesema Marehemu Mrema alikuwa ni kiongozi mkweli na mzalendo kwa taifa ambapo wakati wote alitetea maslahi ya nchi. Amesema taifa limepoteza kiongozi aliyetumikia vizuri nafasi zote alizowahi kuongoza katika uhai wake.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka Saini katika kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema wakati alipofika Nyumbani kwa Marehemu Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Agosti 2022. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Bi. Doreen Kimbi ambaye ni mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema wakati alipofika kutoa pole nyumbani kwa marehemu Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwafariji wanafamilia, viongozi na wanachama wa TLP alipofika msibani nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Agosti 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiongoza sala ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) marehemu Augustine Lyatonga Mrema walipofika msibani nyumbani kwa marehemu Mrema eneo la Salasala Jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Agosti 2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...