JUMLA
ya makarani 8440 wa sensa ya watu na makazi mwaka 2022 Mkoa wa Tanga
wameanza mafunzo yao katika ngazi ya Wilaya yanayotolewa kwa lengo la
kuwawezesha kukusanya takwimu sahihi kutoka kwa wananchi.
Mratibu
wa sensa ya watu na makazi mkoani humo Tony Mwanjota amesema mafunzo
hayo yaliyoanza jana pia wapo wasimamizi wa maudhui 842, na wasimamizi
wa tehama wapatao 245 pamoja na watendaji kata 245 na wote wamehidhuria
katika vituo vya kazi walivyopangiwa.
Mwanjota
alifafanua kwamba katika kila halmashauri ya Mkoa wa Tanga imewekwa
vituo vinne vya mafunzo, huku akisisitiza kuwa, "mafunzo haya yanalenga
kuwawezesha makarani kwenda kukusanya takwimu ambazo zitatakiwa kujazwa
kwenye madodoso" amesema.
"Watu
wanasema tunakwenda kuhesabu watu, lakini siyo hivyo tu bali tuna
takwimu nyingi ambazo tumekusanya ambazo zitakwenda kutusaidia katika
kupanga mipango ya maendeleo yetu, tutaanza kufanya sensa ya watu kwa
siku sita, na baada ya hapo tutajua kukusanya takwimu za majengo kwa
siku tatu" amesema Mwanjota.
Aidha
Mwanjota akitoa wito kwa makarani hao, "kikubwa wazingatie
wanachofundishwa ili waelewe na kuweza kwenda kukusanya takwimu sahihi"
amesema.
Kwa upande wake
Mratibu wa sensa jiji la Tanga Juma Mkombozi amesema katika jiji hilo
kuna vituo katika shule ya sekondari Galanos yenye washiriki 388,
sekondari Usagara washiriki 440, sekondari Mkwakwani washiriki 250 na
sekondari ya Ufundi Tanga washiriki 370, huku wakiwa na watendaji kata
27.
"Mafunzo yameanza
vizuri, tumepokea vifaa vya mafunzo jana na leo mafunzo yanaendelea,
tunatengeneza ndani ya siku 19 mafunzo yatafanyika kwa nadharia na
vitendo,
"Lengo kubwa ni
washiriki wetu wafundishwe namna nzuri ya kwenda kuchukua taarifa
kwenye kaya na maeneo mengine, ikiwemo takwimu za majengo na takwimu za
huduma za jamii katika ngazi ya mtaa" amesema
"Kwahiyo
kwetu sisi tunashukuru mpaka sasa hatuna tatizo lolote lililotupata na
tunatarajia kila kifaa kitafuia kwa wakati ili mafunzo yafanyike kama
ambayo yamepangwa kwenye ratiba yake" amebainisha.
Mkombozi
amesema elimu na hamasa vinatolewa kupitia njia mbalimbali kama Vyombo
vya habari, mikutano ya hadhara kwenye ngazi ya jamii, lakini pia
wanatumia vikao vya kisheri na visivyo vya kisheria kadhalika wanatumia
wasanii kueneza elimu ya sensa.
"Kwahiyo
kila eneo ambalo ni fursa kwetu tunalitumia, lengo ni kuhakikisha watu
wote wanapata elimu, tunachoamini ikifika Agosti 23 kila mtu katika jiji
la Tanga atakuwa amepata elimu na atakuwa tayari kushiriki kwa namna
ambavyo elimu imemfikia" amesema.
Amefafanua
kwamba pamoja na wananchi kujiandaa kuhesabiwa lakini pia watoe
ushiriniano kwa makarani watakapofika katika kaya zao siku itakapofika
kwani ushiriki wao ndiyo utakaosaidia serikali kupata takwimu sahihi
ambazo ndizo zitakakuwa msingi wa ugawaji wa rasilimali za serikali
katika kuleta maendeleo.
Naye
Ofisa mtendaji wa kata ya Pongwe Erika Njana kupitia mafunzo hayo
wameweza kufahamu umuhimu na maana ya sensa na kwamba viongozi wa kata
wanali jukumu kubwa kuhakikisha sensa inafanikiwa kwa kushirikiana na
kamati za kata na mitaa na wengineo.
"Lakini
kupitia sensa, nimeona kabisa kwamba bila kuwashirikisha viongozi hawa
wa chini, itakuwa ni ngumu, kwahiyo sisi tutakwenda kushirikiana moja
kwa moja na viongozi wetu kule chini kuhamasisha jamii kushiriki sensa
kikamilifu" amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...