Mwakilishi wa Jumuiya zisizo za Kiserikali Dkt.  Naufal Mohammed Kassim akitoa salam za waandaaji wa mafunzo ya utoaji huduma Kwa wagonjwa wanaoteseka na maradhi sugu Kwa upande wa Zanzibar, wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kupitia ufadhili wa jumuiya ya wanaoishi na saratani Nchini Oman (OMAN CANSER ASSOCIATION) huko Ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa ndege Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR.

Kiongozi wa Jumuiya ya wanaoishi na Saratani Nchini Oman Dkt.Wahid Al Kharusi akitoa maelezo mafupi kuhusu mafunzo ya utoaji huduma Kwa wagonjwa wanaoteseka na maradhi sugu, na salamu kutoka Kwa wafadhili wa mafunzo wakati wa ufunguzi huko Ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza machache na kumkaribisha mgeni rasmi makamo wa pili wa Rais Mhe.Hemd Suleiman Abdulla kufungua mafunzo ya siku nne ya utoaji huduma Kwa wagonjwa wanaoteseka na maradhi sugu huko Ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.

Na Rahma Khamis  -Maelezo Zanzibar                          

Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe, Hemed Suleiman Abdullah amewataka wananchi kuhamasishana kula vyakula vya mboga mboga na matunda ili kujikinga na maradhi yasioambukiza ikiwemo saratani.

Akifungua mafunzo ya utoaji wa huduma kwa wagonjwa wanaoteseka na maradhi sugu kupitia ufadhili wa Jumuiya ya wanaoishi na saratani nchini Oman huko Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege  amesema maradhi  ya saratani yamekua yakiongezeka siku hadi siku katika jamii hali ambayo inazorotesha afya za wananchi .

Amesema katika kupambana na mradhi hayo Serikali imetenga kiasi cha  bilioni 36.67 kwa lengo la kuimarisha  Afya  za wananchi  kwa kuwapatia matibabu bora kwa kuzingatia mahitaji maalum ya wananchi wake.

Aidha amefahamisha kuwa  mafunzo  hayo ya kuwapatia uwezo madaktari  kuhusu saratani yanakwenda sambamba na uongozi wa awamu ya nane katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya  njema, hivyo yatasaidia wananchi waliowengi kufahamu  matatizo ya ugonjwa huo.

 Makamo ameongeza kwa kusema kuwa Serikali imeamua kujenga Hospitali kila Wilaya zenye uwezo wa kuchukua wagonjwa mia moja kwa wakati mmoja ili wananchi waweze kupata huduma na kua na siha bora.

Hata hivyo amewaasa wanaopatiwa mafunzo hayo kuwa makini na kuyafanyia kazi ili kuhakikisha Afya za wananchi zinaimarika Nchini .

Akitoa takwimu kuhusu ongezeko la maradhi hayo Waziri wa Afya Mhe, Nassor Ahmed Mazurui amesema Zanzibar inawagonjwa 2000 wapya wa saratani mbalimbali ikiwemo matiti, shingo ya kizazi,tumbo na mapafu jambo ambalo linahatarisha afya kwa jamii hivyo ipo haja kuchukua juhudi za makusudi ili kupunguza tatizo hilo.

Aidha amefahamisha kuwa takwimu zinaonesha kuwa jumla ya watu milioni 18 hupata saratani kila mwaka  duniani ambapo milioni 9.6 hufafariki dunia kutokana na maradhi hayo.

Pia ameeleza kuwa katika kuhakikisha wanakabiliana na maradhi hayo Serikali imeanza kuweka tiba ya mionzi na kutengeneza programu ya kwenda Kijiji hadi Kijiji kutoa elimu kuhusu kujikinga ma ugonjwa huo.

Nae Kiongozi wa Oman Cancer Association Dr. Wahid Al-Kharusi  amesema wameamua kutoa mafunzo hayo  na kuwapatia mshine ya kupimia maradhi hayo Zanzibar  ili kuwasaidia wagonjwa hasa wanawake ambao ndio waathirika wakubwa.

Aidha amefahamisha kuwa wataendelea kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kuwapatia mafunzo kila baada ya muda na watakaofanya vizuri kuchaguliwa kuwasomesha wenzao ili Zanzibar iwe na kituo chao wenyewe kitakachotoa huduma hizo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Jumuiya zisizo za Kiserikali Dr Naufal Mohamed Kassim amewaasa wananchi kufika vituo vya Afya mara tu wanapohisi dalili za Saratani kwani Saratani inatibika hasa katika hatua za awali.

Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema watakua makini na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuleta mabadiliko katika Ofisi zao.

Mafunzo hayo  ya siku nne yamewashirikisha madaktari na taasisi zinazoshughulikia maradhi hayo na yametolewa na Jumuiya ya  watu wanaishi na maradhi ya saratani Oman kwa kushirikiana na Kitengo cha maradhi hayo Zanzibar.


Makamo wa Pili wa Rais Mhe.Hemed Suleiman Abdulla  akipokea  zawadi maalum kutoka kwa jumuiya ya wanaoishi na Saratani Nchini Oman mara baada ya kufungua mafunzo ya siku nne ya utoaji huduma Kwa wagonjwa wanaoteseka na maradhi sugu  huko Ukumbi wa Golden tulip Uwanja wa ndege Zanzibar .PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...