Njombe
Baadhi ya wananchi wenye majengo ya kifahari mjini Njombe wametajwa kudanganya taarifa zinazoendana na thamani ya nyumba zao kwa makarani wa sensa ya watu na makazi wakihofia kupandishiwa kodi za majengo.
Msimamizi wa makarani katika kata ya Ramadhani iliyopo mjini Njombe bwana Mussa Seleman ameeleza changamoto hiyo wanayokumbana nayo baadhi ya makarani mbele ya kaimu katibu tawala wa mkoa wa Njombe Ayub Mndeme alipofika katika kata hiyo wakati akikagua maendeleo ya dodoso la majengo.
“Kwenye dodoso kuna kipengele kinachotuhitaji kuingiza thamani ya jengo lakini baadhi ya watu wana mashaka unaona kabisa ana jengo zuri,kubwa la kupendeza na penye thamani kubwa lakini mmiliki anakwambia thamani yake ni milioni tano”amesema Seleman
Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Njombe Ayub Mndeme ametoa wito kwa Wananchi wa mkoa huo kuwa wa kweli kwa kuwa taarifa hizo za majengo zitatumika kwa minajili ya sensa pekee na mipango ya serikali bila kuathiri uchumi wa wamiliki wa majengo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...