Na Jane Edward, Arusha


Baadhi ya taasisi za serikali zilizoshiriki katika maonyesho ya wakulima na wafugaji Kanda ya kaskazini nanenane,wamesema maonyesho hayo yamekuwa na manufaa kwa kuwapatia fursa taasisi hizo kuonyesha watanzania huduma walizo nazo.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa kilele cha maadhimisho ya maonyesho ya kilimo na mifugo nane nane Kanda ya kaskazini yaliyofanyika jijini Arusha.

Wamesema kuwa serikali ilivyobuni uwepo wa sherehe za  wakulima na wafugaji kuonyesha bidhaa zao na huduma wanazotoa kwa jamii ilikuwa ni kumuwezesha mwananchi kujifunza na kuyafanyia kazi ili kuwa na ubunifu zaidi.

Akizungumza na Michuzi blog Profesa Ephafra Manamba anasema wanafundisha wanafunzi kuwa wabunifu ambapo kuna mtambo wa umwagiliaji umebuniwa na vijana wa chuo cha uhasibu njiro na kwamba wakulima wajitokeze kujionea mtambo huo.

"Sisi chuo cha uhasibu tuko vizuri katika kuandaa vijana kujiajiri kama huu mtambo wa umwagiliaji utasaidia vijana kuwafundisha wakulima jinsi ya kutumia na kujipatia kipato" Alisema Profesa Manamba

Amesema mbali na ubunifu huo pia chuo hicho kinamfundisha mwanafunzi jinsi ya kujiajiri na kuajiri watu wengine na kwamba mwanafunzi anapomaliza anakuwa na ujuzi kichwani.

Kwa upande wake afisa mahusiano wa shirika la umeme Tanzania Tanesco Mkoani Arusha James Kuppa amesema katika maonyesho hayo wamekuja na huduma ya Ni-Konekt kwaajili ya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kutumia simu janja kuomba kuunganishiwa umeme.

Amebainisha kuwa katika kuwafikia watanzania wote hususani vijijini wanaendelea kutoa elimu kupitia njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari, Vipeperushi pamoja na kuwafikia ana kwa ana.

Ameongeza kuwa Tanesco kwa sasa inalenga kuiweka dunia kiganjani kwa kutoa huduma zote kidigitali kwa kutumia simu janja na kwa Mkoa wa Arusha wananchi watumie huduma hiyo hata wanapopata changamoto na watahudiwa kwa haraka.

 Profesa Ephafra Manamba Kaimu Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha akipokea zawadi kwa mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere.

James Kuppa afisa mahusiano wa Tanesco Mkoa wa Arusha akitoa maelezo kwa viongozi wa wilaya ya Hai walipotembelea Banda lao.
Pichani Mwenye nyeupe ni mhandisi Shuma meneja wa kanda ya kaskazini Akizungumza na wataalamu wa Umeme katika Maonyesho ya nane nane, alivyotembelea banda la shirika la umeme Tanzania Tanesco.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...