Serikali inajenga mfumo mpya wa Ununuzi ambapo kwa sasa inatumia Mfumo wa Taneps lakini kutokana na changamoto mbalimbali kwenye Mfumo huo, hivyo Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imeamua kuwatumia wataalamu wa ndani ili kujenga Mfumo utakaoweza kutatua changamoto zile zote zilizokuwepo kwenye Mfumo wa zamani.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi amesema changamoto mojawapo ilikuwa ni wafanyakazi kufanya kazi za Ununuzi hata kama hatambuliki na Bodi na alikuwa anaweza kufanya shughuli za Ununuzi bila kukidhi vigezo vilivyowekwa na Bodi hii ilikuwa inapelekea kuwepo kwa madhaifu mengi kwenye shughuli za Ununuzi na wakati wa ukaguzi wa Mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za Serikali alipokuwa anafanya ukaguzi wake alikuwa anakuita madhaifu mengi kwenye Ununuzi wa Umma.

Mbanyi amesema hata wale ambao sio wataalamu wa Ununuzi walikuwa na uwezo wa kutumia Mfumo wa zamani lakini Mfumo huu mpya mtaalamu yoyote hata kama ni Afisa manunuzi Mwandamizi au Afisa manunuzi wa cheo chochote kama hana usajili wa Bodi ya PSPTB hatoweza kuingia kwenye Mfumo huo.

"Mfumo umejengwa kwa minajili kwamba hutoweza kutoka hatua moja kwenda nyingine mpaka uwe umesajiliwa na Bodi hivyo Mfumo huo umeunganishwa na kanzi data ya PSPTB ambapo utaweza kuweka namba ya usajili ili kuendelea na hatua nyingine na kama huna namba ya usajili wa Bodi hiyo hivyo basi utaweza kuendelea na hatua inayofuata" alisema Mbanyi

Mbanyi amesema Wakati Mfumo unaendelea kujengwa na unakaribia kumalizika ili kuingia kwenye majaribio wafanyakazi wanaofanya kazi za Ununuzi waweze kusajiliwa ili Mfumo mpya unapoanza kusiwepo sababu yoyote ya kuchelewesha kazi yoyote ya Serikali.

Pia amesema sasa umefika muda wa kwenda kufanya kaguzi kwa kuangalia wataalamu wanaofanya kazi za Ununuzi maeneo ya kazi kama wamesomea Taaluma hiyo na kama wamekidhi vigezo vyote kama kusajiliwa na Bodi ya PSPTB kwasababu kwenye taarifa za ukaguzi unakuta taasisi fulani imefanya manunuzi chini ya kiwango hii inatokana na wale wanaofanya kazi hizi hawajasomea na hawana sifa stahiki.

Amesisitiza kuwa Bodi ya PSPTB imepewa wajibu kisheria kwa mujibu wa kifungu cha Saba cha Sheria namba 23 ya mwaka 2007, PSPTB imepewa Mamlaka ya kisheria ya kuhainisha vigezo vya kitaaluma katika utendaji kazi katika tasnia ya Ununuzi na Ugavi.

Tutapita Kukagua kuangalia je wanaofanya maamuzi katika Taasisi na makampuni binafsi je ni watu wenye sifa stahiki kwaiyo hilo ni jukumu litakaloanza kutekelezwa kuanzia tarehe 13 mwenye Septemba mwaka huu kama kwenye wanasufa stahiki na Bodi inawatambua alisema Mbanyi
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mkutano wa Bodi hiyo Leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...