*Ampongeza Rais Samia kwa kuweka zaidi ya Sh.bilioni 100 ujenzi vituo vya umahiri
Na Mwishehe, Michuzi TV
KATIBU
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka
amesema Chama hicho kinaipongeza Taasisi ya Teknolojia Dar es
Salaam(DIT) kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhakikisha gesi asili
inatumika kuendesha vyombo vya moto kama magari ili kupunguza gharama
kubwa ya fedha inayotumika kununua mafuta nje ya nchi.
Aidha
amesema Chama kinampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha
nyingi kiasi cha zaidi ya Sh.bilioni 100 kwa ajili ya kuiwezesha DIT
kujenga vituo vya umahiri ambavyo vitakuwa chachu ya kupika watalaamu wa
kada mbalimbali wakiwemo watalaamu wa kufunga mifumo ya gesi kwenye
magari yanayotumia mafuta ya petroli na dizeli.
Shaka ameyasema
hayo leo Agosti 29,2022 alipofanya ziara fupi ya kutembelea DIT kwa
lengo la kuwapongeza na kuwatia moyo kwa kazi nzuri wanayofanya ya
kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2020/2025 ambayo
inaelezea kwa kina kuhusu uwekezaji kwenye eneo la TEHAMA.
“Kumekuwa
na jitihada kubwa zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi kupitia Serikali
ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia kwenye uwekezaji wa fedha nyingi za
maendeleo maeneo mbalimbali .Moja ya eneo ambalo pengine hatujafika
kuona namna ambavyo fedha zimewekwa na utekelezaji unaendelea ni eneo
hili lililobeba teknolojia
“Nikisema teknolojia tunaamanisha
mfumo mzima wa mabadiliko haya ya kidunia na hapa nazungmzia TEHAMA, leo
tumepata fursa hii kuona namna ambavyo wenzetu wa DIT wanatumia
utaalamu huu kubadilisha miundombinu hii ya magari kutoka kwenye mafuta
kwenda kwenye gesi.
“Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kueleza
kujitegemea ni kwa maana kutumia fursa vizuri kulinufaisha taifa , sasa
moja ya fursa tuliyonayo ni gesi asilia ambayo imegundulika na imeanza
kutumika , tunaelezwa tunayo akiba ya karibia futi trilioni 57 .5 ambayo
imeifanya Tanzania kuwa nchi ya 82 duniani kwa utunzaji na umikili wa
gesi asili,”amesema Shaka.
Amefafanua gesi asili imeshaanza kutumika kwa kiasi fulani kwa matumizi ya uzalishaji wa umeme lakini kwa matumizi ya viwandani
“Sasa
tumekuwa tukijitanua kwenye suala zima la teknolojia , nichukue fursa
hii kuwapongeza DIT kwa namna wanavyotafsiri dhana lakini kwa kusimamia
na kuhakikisha kifungu cha 63 C cha Ilani ya Uchaguzi Mkuu
kinatekelezeka.Bahati nzuri wanayoyatekeleza DIT sio matakwa yao ama
utashi wao bali wanatekeleza Ilani ya CCM,”amesema Shaka.
Ameongeza kwa niaba ya Chama hicho wanampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo Sh.bilioni 100 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa vituo vya umahiri kwenye eneo hili.
“Kwa kiasi kikubwa kama likisimamiwa vema katika vita hii ya uchumi inayoendelea hivi sasa DIT ni kamandi muhimu katika mapambano ya uchumi.Hivyo hawa wenzetu walipewa dhamana wakifanya kazi yao vizuri matokeo yake yatakuwa makubwa na yenye tija kubwa kwenye taifa letu,”alisema Shaka.
Amesema kwanza itapunguza matumizi ya mafuta kwenye magari ,hivyo teknolojia hiyo itasaidia kupunguza matumizi ya fedha nyingi zinazotumika kununua mafuta lakini itasaidia kwenye suala la usafirishaji endapo uhamasishaji ukafanywa vizuri na wafanyabiashara wa ndani wakahamasishwa.
“Na Serikali yenyewe ikajipanga kwenye kujenga vituo vya kusambaza hiyo gesi asili. Hatua ya kwanza wanafunga mifumo kwenye magari na hatua ya pili ni kuwa na vituo kadhaa vitakavyosaidia sasa kutoa fursa pana zaidi ili wale ambao watakuwa wanatumia gesi hii kusiwe na usumbufu , tunakuwa tumepiga hatua kubwa katika dhana ya maendeleo endeleo.”
Aidha amesema teknolojia hiyo itafanya Tanzania kutumia vizuri fursa hiyo ya kidunia kama ambavyo ameeleza nchi yeti iko katika nchi 82 sio jambo dogo. “Lazima tufanye vizuri kwenye suala la taaluma na kwenye hili nadhani ndio msingi wetu mkubwa kuwa na watalaamu wa kutosha watakasimamia dhana hii.
“Tumeanza na tuna imani kwamba itakuwa na mafanikio makubwa lakini huu nadhani ni mlango mwingine wa kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.Naamini endapo mipango na mikakati thabiti itawekwa ni sehemu mojawapo ambayo tutaweza kuwaanda vijana wetu kutumia fursa hii ambayo imeibuliwa kuwatoa kwenye kilio cha ukosefu wa ajira ajira kwa vijana,”amesema Shaka.
Ameongeza teknolojia hiyo itatutoa kwenye utegemezi wa mafuta kama Taifa lakini si utegemezi wa mafuta tu sasa watalaamu waje na mawazo mapya na utalaamu wao utumike kushauri na maeneo mengine huko kwenye bajaji, boda boda, nako pia tukipeleka teknelojia hii na tutakuwa tumewasaidia sana vijana.
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka akipata maeelezo kutoka kwa Meneja wa Mradi wa Kuunganisha Mfumo wa Gesi Asili katika Magari (CNG), Dkt. Esebi Nyari,namna vipuri vya mifumo ya gesi inavyounganishwa kwenye magari mbalimbali,alipofanya ziara fupi ya kutembelea DIT kwa lengo la kuwapongeza na kuwatia moyo kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2020/2025 ambayo inaelezea kwa kina kuhusu uwekezaji kwenye eneo la TEHAMA.
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka akipata maeelezo kutoka kwa Meneja wa Mradi wa Kuunganisha Mfumo wa Gesi Asili katika Magari (CNG), Dkt. Esebi Nyari,namna mifumo ya gesi inavyounganishwa na kufanya kazi kwenye magari mbalimbali,alipofanya ziara fupi ya kutembelea DIT kwa lengo la kuwapongeza na kuwatia moyo kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2020/2025 ambayo inaelezea kwa kina kuhusu uwekezaji kwenye eneo la TEHAMA.
Meneja wa Mradi wa Kuunganisha Mfumo wa Gesi Asili katika Magari (CNG), Dkt. Esebi Nyari akitoa ufafanuzi kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka kuhusu mifumo ya gesi inavyounganishwa na kufanya kazi kwenye magari mbalimbali. Shaka amefanya ziara fupi ya kutembelea DIT kwa lengo la kuwapongeza na kuwatia moyo kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2020/2025 ambayo inaelezea kwa kina kuhusu uwekezaji kwenye eneo la TEHAMA.
Kikao kikendelea
MKurugenzi Mkuu wa Kampuni Tanzu ya DIT John Msumba akifafanua mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo kampuni hiyo inavvyofanya kazi ikiwemo na kutoa elimu kwa vitendo kwa Wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho
Mkuu wa Taasisi ya DIT Prof.Preksedius Ndomba akizungumza jambo mara baada ya kumkaribisha Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka aliyefanya ziara fupi ya kutembelea DIT kwa lengo la kuwapongeza na kuwatia moyo kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2020/2025 ambayo inaelezea kwa kina kuhusu uwekezaji kwenye eneo la TEHAMA. Picha na Michuzi JR.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...