MKUU wa mkoa wa Iringa Halima Dendego amewataka wakurugenzi wa halmashauri mkoani Humo kubuni vyanzo vya mapato na kuboresha vyanzo vilivyopo ili kuwezesha Halmashauri kuweza kuongeza uwezo wa kujitegemea kwa mapato ya ndani ya halmashauri.
Amesema hayo wakati akizungumza na watumishi wa mkoa mara baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Queen Sendiga ambaye amehamishiwa mkoa wa Rukwa.
Halima amesema ni vyema kila mkurugenzi kuweka mkakati wakuwa na chanzo kingine cha mapato ili kusaidia kuwahudumia wananchi katika nyanja mbalimbali.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego akikabidhiwa ofisi na Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Qeen Sendiga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...