
Njombe
MTOTO wilayani Makete mkoa wa Njombe amekutwa amefariki kwa kujiua kutokana na kunywa sumu baada ya kuonywa kwa kukalipiwa na baba yake aliyekuwa akimuonya baada ya kuwaacha Punda waliokwenda kula mazao kwenye shamba la watu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema mtoto huyo aliacha Punda aliokuwa nao machungoni na kwenda kucheza na watoto wenzake hali iliyomfanya baba yake kumuonya baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mwenye shamba.
“Huyu mtoto alipewa Punda akachunge,akawaacha na akaenda kucheza na matokeo yake wale punda wakala shamba la mtu,mzee wake akalalamikiwa ndipo akamuita mtoto lakini kitendo cha mzee kumfokea yule mtoto achunge punda kwa umakini,yeye akachukua maamuzi magumu akatafuta simu akanywa na kufariki”Amesema Kamanda Issah
Kamanda Issah ametoa wito kwa wazazi na walezi kutafuta njia sahihi ya kuzungumza na watoto huku pia akiomba makanisa kuendelea kutoa mafunzo mema ya dini ili kutokuwa na maamuzi magumu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...